Thursday, December 26, 2013

Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe-Utumishi uliotukuka mwaka 2012

TANZANIA inatarajia kupata mgawo wa takribani shilingi bilioni 400 kutokana na mauzo ya hisa yaliyofanywa na kampuni ya Ophir kwa kampuni ya Pavillion katika vitalu vya gesi vilivyopo nchini, Raia Mwema limeambiwa.

Kampuni ya Ophir inamiliki asilimia 40 ya hisa katika vitalu namba 1, 3 na 4 huku asilimia nyingine 60 ikimilikiwa na kampuni ya BG lakini Ophir wameamua kuuza hisa zao 20 mwaka huu.

Mauzo ya hisa hizo yanatarajiwa kuiingizia Ophir kiasi cha dola bilioni 1.3 (shilingi trilioni mbili) na kutokana na mauzo hayo, Tanzania itapata kiasi cha dola milioni 260 (shilingi bilioni 400) kama kodi.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Tanzania kufaidika na mauzo ya hisa za rasilimali zake kupitia Kodi ya Ongezeko la Mtaji (Capital Gain Tax) ambayo ilipitishwa na Bunge mwaka jana.

Kodi hiyo ilipitishwa na Sheria ya Fedha (Finance Act) ya mwaka 2012 baada ya kuwasilishwa kama mapendekezo binafsi na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe na kuridhiwa na Bunge.

Katika miaka ya nyuma, Tanzania haikuwa ikifaidika na mauzo yoyote ya hisa kwa makampuni yanayouziana rasilimali zake kwa sababu Kodi hiyo ya Ongezeko la Mtaji haikuwepo.

Utumishi uliotukuka......

No comments:

Post a Comment