ZIARA YA KATIBU MKUU DKT. WILLIBROD
SLAA
Katibu
Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa
ataanza ziara ya siku 20 katika mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida kuanzia
Desemba 4-23, mwaka huu.
Lengo
la ziara hiyo ambayo imetokana na maombi ya muda mrefu ya viongozi wa chama
katika maeneo husika, ni kuimarisha na kukagua uhai wa chama katika ngazi za
chini hususan kata na majimbo mikoa hiyo.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakutana na wananchi katika
mikutano ya hadhara ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya kitaifa na eneo
husika, kisha atafanya vikao vya ndani vya kichama.
Ziara hiyo itaanzia mkoani Shinyanga ambapo siku ya Jumatano Desemba 4,
mwaka huu, Katibu Mkuu Dkt. Slaa atakuwa Wilaya ya Kahama, siku inayofuata
Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa
Jimbo la Muhambwe.
Ratiba ya siku zinazofuata itaendelea kutolewa kwa vyombo vya habari.
Imetolewa leo Jumanne, Desemba 3,
2013, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari CHADEMA
No comments:
Post a Comment