Bayern Munich inafunga mwaka wa
2013 kwa kutwaa Kombe la Klabu Bingwa duniani baada ya kupata ushindi
dhidi ya mabingwa wa Morocco, Raja Casablanca katika mchezo uliochezwa
mjini Marrakech, Morocco.
Mabingwa hao wa Ujerumani wameongeza kombe
lingine katika mkusanyiko wa makombe waliyoyatwaa likiwemo la klabu
bingwa ya ligi ya Bundesliga,Ujerumani na kombe la Uefa katika mwaka huu
wa mafanikio.Dante na Thiago Alcantara walifunga mabao hayo mawili na kuandikisha ushindi kwa timu ya Bayern.
Bayern Munich mabingwa wa dunia |
Bayern walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa kombe hilo kwa kuwachapa Raja ambao matarajio yao yalizidi hatua ya kufikia fainali katika mchezo uliochezwa nchini mwao Morocco.
Timu hiyo ya Morocco ambayo ilishangiliwa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza katika uwanja wa nyumbani wa Marrakach, walichukuliwa kuwa timu dhaifu kuliko zote katika michuano hiyo ya kuwania ubingwa wa dunia kwa vilabu. Lakini waliwatoa Auckland City, Monterrey na timu ya Ronaldinho, Atletico Mineiro.
Kwa upande wao timu ya Bayern iliicharaza Guangzhou Evergrande mabingwa wa bara la Asia, huku mabingwa hao wa Ulaya wakiingia hatua ya nusu fainali. Waliwatandika Guangzhou 3-0 huku wakipata urahisi wa kuwacharaza Raja mabao 2-0 katika muda wa robo saa ya mchezo.
No comments:
Post a Comment