Wapiganaji wa Boko Haram
wameshambulia ngome ya kikosi cha anga cha Jeshi Kaskazini Mashariki mwa
Nigeria na kuharibu helkopta mbili maafisa wa serikali wamesema.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema mamia ya
wapiganaji wameshambulia maeneo kadhaa katika mji wa Maiduguri kuanzia
mapema asubuhi siku ya jumatatu.Amri ya kutotembea ovyo ya saa 24 imetangazwa katika jimbo la Maiduguri. Na uwanja wa ndege unaotumiwa na wananchi umefungwa kwa muda.
Mwandishi wa habari wa BBC anasema shambulio hilo lililopangwa ni shambulio kubwa ambalo limerudisha nyumba juhudi za Jeshi la Nigeria.
Maelfu ya watu wameuwawa nchini Nigeria na wapiganaji hao tangu mwaka 2009 wakati Boko Haram walipoanza mashambulizi ya kutaka kusimika utawala unaoegemea sharia ya kiislamu.
No comments:
Post a Comment