Wednesday, December 11, 2013

Hayati Mandela aendelea kumiminiwa sifa

Mwili wa Mandela ukisindikizwa na polisi Afrika Kusini
Mwili wa aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini Marehemu Nelson Mandela umewasili kwenye ikulu ya Afrika Kusini mji Mkuu wa Pretoria, na utalala hapo kwa siku tatu.
Mwili ulichukuliwa katika msafara kutoka chumba cha maiti cha hosptali hadi kwenye jengo la Muungano.
Msafara wenye jeneza la Marehemu uliondoka mjini katika Hosptali ya jeshi muda mfupi siku ya jumatano. Jeneza lilibebwa kwenye gari maalum na kufunikwa bendera ya Afrika Kusini.
Wananchi walijipanga kando kando ya barabara lilipopitishwa jeneza kama ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Msafara ulipita katika mitaa huku baadhi ya raia wakikimbia pembeni kwenye mstari wa askari wa wanajeshi Mwandishi BBC's Joseph Winter katika mji wa Pretoria amesema.
Wanajeshi waliobeba jeneza hilo walisonga hatua kwa hatua hadi katika Majengo ya Muungano eneo alikoapishwa kuwa rais wa kwanza mzalendo wa Afrika kusini 1994.
Wanachi, wakuu wa nchi walioalikwa na wageni wengine wa kimataifa watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu aliyefariki alhamisi akiwa na umri wa miaka 95.
Wageni hata hivyo hawaruhusiwa kupiga picha.
Leo jioni wasanii mbali mbali wa Afrika Kusini watashiriki katika tamasha maalum la kumuenzi Mandela na ambalo wananchji wataruhusiwa kuhudhuria bila malipo.
Marehemu Mandela atazikwa nyumbani kwake katika kijiji Qunu katika jimbo la Cape Mashariki siku ya jumapili.
Maelfu ya raia wa Afrika ya kusini hapa jana waliungana na viongozi mbali mbali duniani katika ibada ya kumbu kumbu siku ya jumanne kama sehemu ya mfululizo wa maombolezo kifo chicho.

No comments:

Post a Comment