Viongozi kutoka Afrika mashariki
wanatarajia kukutana nchini Kenya kujadili kuhusu machafuko
yanayokithiri nchini Sudani kusini, ambapo zaidi ya Watu 1,000
wanaaminika kupoteza maisha.Mazungumzo hayo yanakuja siku moja baada ya
Rais wa Sudani kusini Salva Kiir kukutana na Mawaziri wakuu kutoka
nchini Kenya na Ethiopia.
Wakati huo huo Umoja wa Mataifa umesema kuwa
kikosi cha kwanza cha kulinda amani kinatarajiwa kuwasili nchini Sudani
kusini saa kadhaa zijazo.machafuko yalijitokeza siku 12 zilizopita kati
ya vikosi vinavyomuunga mkono Kiir na vile vinavyomuunga mkono aliyekuwa
naibu wa Kiir, Riek Machar. Zaidi ya raia 50,000 wamekimbia makazi yao
na kuomba hifadhi katika Ofisi za UN huko Sudani kusini.Rais wa Sudani kusini Salva Kiir |
Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Habari wa Sudani kusini Makuei Lueth ameliambia shirika la habari la AP kuwa mpaka sasa hakuna mawasiliano na Machar.
Sudani kusini imekuwa ikipigania kupata Serikali thabiti tangu kupata uhuru wao mwaka 2011, baada ya kujitenga.
No comments:
Post a Comment