Operesheni Tokomeza-ilikuwa kama ifuatavyo
, Operesheni Tokomeza ilihusisha jumla ya washiriki 2,371 kutoka vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa mgawanyo ufuatao:-
i. Wanajeshi (885) kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania,
ii. Askari (480) kutoka Jeshi la Polisi,
iii. Askari (440) kutoka Kikosi Dhidi ya Ujangili (KDU)
iv. Askari Wanyamapori (383) kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)
v. Askari (99) kutoka Wakala wa Huduma za Misitu (TFS)
vi. Askari Wanyamapori (51) kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)
vii. Waendesha Mashitaka (23) na
viii. Mahakimu (100
…Operesheni ilikuwa ya kijeshi. Ilikuwa ya kijeshi kwa sababu
ilitekelezwa kwa amri ya jeshi Namba 0001/13 iliyotolewa tarehe 28
Septemba, 2013 na kusainiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi…”
Kamati
ilifanya mikutano mbalimbali katika baadhi ya maeneo ilikofanyika
Operesheni Tokomezakwa lengo la kuwasilikiliza waathirika na kubaini
mambo yafuatayo:-
Watuhumiwa kupekuliwa, kudhalilishwa na baadhi kutojulikana walipo
i. Mheshimiwa Spika, badhi ya wananchi wakiwemo viongozi, Madiwani na
Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji na Watumishi wa Serikali walikamatwa na
kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza. Baadhi ya watuhumiwa
waliokamatwa walikuwa hawajulikani walipo hadi Kamati ilipozuru maeneo
hayo. Mfano; Vijana watatu wa Kijiji cha Osteti, Kata ya Chapakazi,
Wilayani Kiteto, walituhumiwa kujihusisha na biashara ya Meno ya Tembo.
Vijana hao ni Nyafuka Ng’onja, Ng’onja Kipana na Mswaya Karani.
ii.
Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa walidai kudhalilishwa mbele ya
wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu za
siri bila ridhaa yao. Mfano; ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi,
Wilaya ya Ulanga alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa
na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanae wa kiume (11) akishuhudia.
Pia alidai kulazimishwa kuchora picha ya Chatu kwa kutumia wembe kwenye
paja lake. Vilevile, Bi. Neema Moses wa Babati alidai kuvuliwa nguo na
kulazimishwa afanye mapenzi na wakwe zake na pia kuingizwa chupa sehemu
zake za siri.
Aidha, baadhi ya akina mama walidai kubakwa na
kulawitiwa. Mfano; katika Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, mwanamke
mmoja alidai kubakwa na Askari wawili (2) wa Operesheni Tokomeza
Ujangili mida ya usiku. Vilevile, mama mmoja mkazi wa Kata ya Matongo
Wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu (3) wa Operesheni Tokomeza
Ujangili huku akiwa ameshikiwa mtutu wa bunduki
iii. Watuhumiwa
waliokamatwa walifanyiwa upekuzi bila kuhusisha viongozi wa Serikali za
maeneo husika na kutokuwepo kwa mashahidi na hati za upekuzi.
Mfano; Ndg. Abdallah Pata na Bi. Flora Mwarabu wa Kata ya Iputi Wilayani
Ulanga na Ndg. Elias Cosmas Kibuga wa Gallapo Babati, walipekuliwa bila
kufuata utaratibu.
Ukatili na Udhalilishaji katika Kambi za Mahojiano
iv. Mheshimiwa Spika, baadhi ya watuhumiwa waliopelekwa katika kambi za
mahojiano walidai kuteswa kwa adhabu zinazokiuka haki za binadamu.
Mfano; Diwani wa Kata ya Sakasaka wilaya ya Meatu Ndg. Peter Samwel,
alidai kuadhibiwa akiwa mtupu kwa kupewa adhabu za kijeshi kama
kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa vyuma na kulazimishwa
kufanya mapenzi na mti.
Mheshimiwa Spika, kutokana naukatili
uliopitiliza, baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa majina kama vile
Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajega (Serengeti).
No comments:
Post a Comment