Tuesday, December 10, 2013

Uchaguzi mdogo madiwani Februari 9 2014

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza kuwa uchaguzi mdogo wa kujaza viti vilivyo wazi vya madiwani katika kata 27 zilizoko halmashauri 23, utafanyika Februari 9, mwakani.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Julius Malaba, alisema kuwa viti hivyo vimekuwa katika kata hizo kutokana na baadhi ya madiwani kufariki dunia na wengine kupoteza sifa.
Kata hizo na halmashauri zake ni:

Na Kata Halmashauri
1 Segela Chamwino
2 Mpwayungu
3 Ukumbi Kilolo
4 Ibumu
5 Nduli Iringa
6 Malindo Rungwe
7 Santilya Mbeya
8 Tungi Morogoro
9 Mkwiti Tandahimba
10 Mkongolo Kigoma
11 Sombetini Arusha
12 Mrijo Chemba
13 Magomeni Bagamoyo
14 Kibindu
15 Mtae Lushoto
16 Ubagwe Ushetu
17 Namikago Nachingwea
18 Partimbo Kiteto
19 Loolera
20 Kiwalala Lindi
21 Kilelema Buhigwe
22 Kiomono Tanga
23 Kasanga Kalambo
24 Rudewa Kilosa
25 Kiboroloni Moshi
26 Njombe Mjini Njombe
27 Nyasura Bunda

Uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Januari 15, wakati kampeni za uchaguzi zitaanza Januari 16 hadi Februari 8 na siku ya kupiga kura itakuwa Februari 9, mwakani.
Zoezi la uwekaji wazi Daftari la Kudumu la Wapiga kura litafanyika kuanzia Februari mosi, mwakani katika vituo walivyojiandikisha wapiga kura wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na zoezi hilo litafanyika kwa siku saba.
Wagombea wa udiwani watachukua fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi kuanzia Januari 2 kabla ya saa 10:00 alasiri.
Wagombea wanatakiwa kuwasilisha fomu za uteuzi kwa msimamizi wa uchaguzi siku ya uteuzi katika muda usiozidi saa 10:00 alasiri.

Source: NIPASHE Jumatano Desemba 4, 2013

No comments:

Post a Comment