Johannesburg.
Serikali ya Afrika Kusini, imetoa orodha ya majina ya wakuu wa nchi na
Serikali 91 ambao wamethibitisha kushiriki katika shughuli zinazohusiana
na safari ya mwisho ya Rais wa kwanza mzalendo wa taifa hilo, Nelson
Mandela.
Jina la Rais Jakaya Kikwete ni la kwanza katika orodha hiyo inayowaweka
viongozi hao katika makundi kutokana na mabara wanakotoka. Rais Kikwete
alitarajiwa kuwasili jana usiku tayari kuhudhuria Ibada ya Kitaifa ya
Mandela ambayo imepangwa kufanyika leo kwenye Uwanja wa FNB (Soccer
City).
Kabla ya Serikali kutoa orodha hiyo,Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa wa
Afrika Kusini, Maite Nkoana-Mashabane alisema wakuu wa nchi na Serikali
53 walikuwa wamethibitisha lakini jana mchana idadi hiyo ilikuwa
imeongezeka na kufikia 91. Kulikuwa na wasiwasi kwamba huenda idadi hiyo
ikaongezeka na kuzidi 100.
Msemaji wa Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa ya Afrika Kusini, Clayson
Monyela aliwataja marais wengine kutoka Afrika kuwa ni kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Kongo (DRC),Joseph Kabila, Hifikepunye Pohamba wa
Namibia, Mike Sall wa Senegal,Allessane Ouattara wa Cote
d’Ivoire,Goodluck Jonathan wa Nigeria,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Dennis
Sassou-Nguesso wa Congo Brazaville, John Dramani wa Ghana na Ali Bongo
wa Gabon.
Kutoka Amerika ya Kusini ni marais Nicolus Maduro Moros wa Venezuela na
Dilma Rousseff wa Brazil ambaye ataambatana na marais wanne wastaafu wa
nchini kwake.
Waziri Mkuu wa Bahamas, Perry Christie, Rais wa Guyana, Donad Ramotar,
Rais wa Haiti, Michael Martelly na Rais wa Jamaica, Portia Miller,
wakati kutoka Asia, kutakuwa na marais Pranab Mukherjee wa India na
Hamid Karzai wa Afghanistan.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa,Waziri Mkuu wa Australia, Tony Abbot,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon Tayari Rais wa Marekani,
Barrack Obama na mkewe Michelle walishathibitisha kushiriki, pia
watangulizi wake, Bill Clinton,George W. Bush na Jimmy Carter
wanatarajiwa kushiriki katika mazishi ya Mandela yatakayofanyika Qunu,
Mthatha Jumapili.
Armando Guebuza wa Msumbiji, Abdelkader Bensalah wa Algeria,Makamu wa
Rais wa Angola, Manuel Vicente, Rais wa Niger, IssoufouMahamdou, Kaimu
Rais wa Agentina,Amado Boudou, Waziri Mkuu wa New Zealand, John Key na
Rais wa Bangladesh, Abdul Hamid MD Abdul.
Malkia Haakon wa Norway, Mfalme wa Philippe wa Ubelgiji, Rais wa
Pakistan, Mamnoon Hussain, Rais wa Benin, Boni Yayi, Rais wa Palestina
Mahmoud Abbas, Rais wa Botswana,Seretse Ian Khama, Rais wa Ureno,Anibal
Cavaco Silva na Mfalme wa Saudi Arabia, Muqrin bin Abdulaziz Al-Saud,
Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza, Rais wa Saharawi,Mohamed Abdelaziz,
Waziri Mkuu wa Canada,Stephen Harper wa Chad, Idriss Deby Itno, Rais wa
Serbia, Tomislav Nikolic,Makamu Rais wa China, Yuanchao,Rais wa
Shelisheli, James Alix Michel,Rais wa Comores, Dr Ikiliou Dhoinine na
Mfalme wa Hispania, Felipe de Borbon.
Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapaksa,Makamu Rais wa Sudan, Hassan
Salih,Rais wa Suriname, Desire Delano Bouterse, Rais wa Slovenia,
Pahor,Rais wa Croatia, Josipovic Ivo, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kir
Mayardit, Rais wa Cuba, Raul Castro Ruz, Rais waDjibouti, Ismail Omar
Guelleh, WaziriMkuu wa Swaziland, Dr Sibusiso Dlamini, Waziri Mkuu wa
Ethiopia, Ato Hailemariam Dessalegn na Rais wa Equatorial Guinea, Obiang
Mbasogo.
Rais wa
Finland, Sauli Niinisto, Rais wa Tunisia, Mohamed Moncef Marzouki,
Waziri Mkuu wa Trinidad na Tobago, Kamla Persad-Bissessar, Rais wa
Gambia, Prof Alhaji Dr Yahya Jammeh, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,
Rais wa Ujerumani,Joachim Gauck, Rais wa Guyana,Donald Ramotar, Rais
Michael Satta wa Zambia na Rais wa Guinea,Profesa Alpha Conde.
Mwanamuziki Bono, Mtangazaji,Oprah Winfrey na Mwanamitindo,Naomi
Campbell na watoto kutoka Familia ya Malkia wa Uingereza,Prince Charles
na Prince Harry.
No comments:
Post a Comment