Taarifa
za awali ambazo zilianza kusambaa zilikuwa zikidai kuwa ni hoteli ya
Kilimanjaro Kempisk ndio iliyokuwa ikiungua na kusababisha waandishi wa
habari pamoja na baadhi ya wakazi wa jiji kufika katika eneo hilo na
baadae kubaini moshi mkubwa ukifuka kutoka katika mojawapo ya majengo ya
benki kuu ya Tanzania ambapo baadhi ya askari wa jeshi la polisi pamoja
na wananchi wamekusanyika kuishuhudia hali hiyo.
Kitambo
kidogo baada ya wananchi kukusabyika baadae kikosi cha zimamoto nacho
kikawasili katika eneo la tukio tayari kabisa kukabiliana na hatari ya
moto ambapo hata hivyo walilazimika kuondoka katika eneo la tukio huku
kiongozi wa msafara huo aliyejitambulisha kwa jina la sifuri simba
akidai kuwa wamepata taarifa ya uwepo wa tukio la moto katika benki kuu.
Kamanda
wa polisi mkoa wa kipolisi wa Ilala Marietha Minangi ameviambia vyombo
vya habari kuwa hakuna tukio lolote la ajali ya moto bali ni jenereta la
benki hiyo lilikuwa likijiwasha mara baada ya kukatika kwa umeme wa
Tanesco.
Hata
hivyo maelezo ya kamanda huyo yanatofautiana na maelezo ya mmoja wa
walinzi wa benki hiyo ambaye hakutaka kupigwa picha wala kutaja jina
lake kuwa moshi huo umesababishwa na zoezi la kawaida la kusafisha
mtambo ambao hata hivyo alikataa kuutaja mtambo huo uliokuwa ukisafishwa
ni wa shughuli gani.chanzo ITV
No comments:
Post a Comment