Sunday, January 12, 2014

Halmashauri ya Jiji la Arusha limeongeza ukusanyaji mapat



Halmashauri ya Jiji la Arusha limeongeza ukusanyaji mapato, kutoka Sh. milioni 400 hadi milioni 927, Desemba, mwaka jana, kutoka vyanzo vyake vya ndani.

Mafanikio haya yametokana na matumizi ya mfumo wa Epicol.Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Sipora Liana, alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kazi katika jiji hilo, mbele ya kamati ya kudumu ya hesabu za serikali za mitaa iliyotembelea halmashauri hiyo kwa siku mbili.

Liana aliiambia kamati hiyo iko katika ziara ya kikazi kuangalia utendaji wa shughuli za maendeleo katika jiji hilo likiwemo suala la upangaji wa mipango ya maendeleo,ukusanyaji wa mapato na usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha.

Alisema jiji la Arusha limenunua
mitambo ya barabara kwa Sh. milioni 740.3 na kugharamia ujenzi wa madarasa zaidi ya 39,katika shule za sekondari ambao ukikamilika utagharimu zaidi ya Sh. bilioni 1.2 kabla ya Januari 31, mwaka huu.

Alisema kutokana na kuboreshwa kwa ukusanyaji wa mapato ya ndani, jiji limelipa madeni ya walimu, ambapo zaidi ya Sh. milioni 22.5 zimetumika.
Alisema jiji limelipa posho zote za wenyeviti wa mitaa kwa kutumia mapato ya ndani.

Alisema kwa mwaka 2013/2014, halmashauri ya ilikadiria kukusanya na kupokea Sh. bilioni 47.2.Katika kipindi cha Julai na Desemba 2013 mapato ya ndani na serikali kuu yalifikia Sh. bilioni 15.7 sawa na asilimia 33.3 ambapo matumizi yalifikia Sh. bilioni 13.9 sawa na asilimia 29.7

Aliiambia Kamati hiyo kwamba mfumo huo wa Epical umesaidia kuwepo na usimamizi mzuri na matumizi ya fedha katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kuzingatia bajeti iliyoidhinishwa Aidha i liana ametaja faida nyingine za mfumo huu kuwa hakuna malipo yanayofanyika nje ya mfumo na pia hauruhusu malipo yafanyike kama fedha hazijapoklewa na kuingizwa katika vifungu husika

Mkurugenzi Liana pia alisema kwamba mfumo huu umerahisisha utoaji wa taarifa za fedha kwa usahihi zaidi na kwa wakati.

Naye Mwenyekiti wa Kamati hiyo na mbunge wa Jimbo la Ole Pemba,Rajabu Mbarouk, ameupongeza uongozi wa jiji la Arusha kwa kuwa moja ya majiji yaliyofanikiwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya serikali na matumizi yake kwa nidhamu ya hali ya juu.

Alisistiza umuhimu wa mfumo huo wa Epical katika kufanikisha mkakati wa serikali wa ukusanyaji wa mapato na matumizi yake.

CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment