Friday, December 27, 2013

Arsenal yarejea tena kileleni mwa ligi


Theo Walcott alifunga magoli mawili naye Luka Podolski alifunga la tatu na kuisaidia Arsenal kutoka nyuma na kuishinda West Ham katika uwanja wao wa nyumbani na kurejea tena kileleni mwa ligi kuu ya Premier.
Arsenal ilitawala kipindi cha kwanza lakini Carlton Cole aliifungia West Ham bao lake la Kwanza baada ya kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny kutema mpira kwenye eneo la hatari
West Ham ilipoteza nafasi nyingi za kufunga hali iliyompa Walcott kusawazisha.
Muda mfupi baadaye Podolski alimpa Walcott pasi nzuri ambaye aliitia kimyani na kuiweka Arsenal mbele kwa magoli mawili kwa moja.
Luka Podolski na Theo Walcott wakisherehekea
Kufuatia matokeo hayo West Ham sasa imeshuka hadi nafasi ya kumi na saba alama moja tu mbele ya timu tatu zinazoshikilia nafasi za mwisho.
Timu hiyo imeshinda mechi moja tu kati ya mechi kumi na moja zilizopita na itakuwa na kibarua kigumu kubadili matokeo hayo wakati itakapochuana na West Brom siku ya Jumamosi.
Arsenal sasa inaongoza ligi hiyo na alama thelathini na tisa alama moja nyuma ya Manchester City ambayo iliilaza Liverpool kwa magoli mawili kwa moja.
Chelsea inashikilia nafasi ya tatu na alama thelathini na saba kufuatia ushindi wake wa bao moja kwa bila dhidi ya Swansea.

No comments:

Post a Comment