Wednesday, December 11, 2013

Taarifa kwa vyombo vya habari


Baada ya kupokea barua yake ya mashtaka 11 tarehe
01/12/2013 ambayo anashitakiwa nayo na iliyomtaka ajitetee
kwa maandishi, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) jana
tarehe 10/12/2013 amefanya hivyo kwa mujibu wa Katiba na
Kanuni za Uendeshaji za Chama.
Pia Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe (MB) ametoa taarifa kwa
Katibu Mkuu wa Chama kumueleza nia yake kukata rufaa
Baraza Kuu la Chama kupinga hatua iliyochukuliwa na Kamati
Kuu dhidi yake kumvua nyadhifa zake ndani ya Chama.
Kuna sababu mbili za msingi za kukata rufaa;
1. Utaratibu wa kuchukua hatua za nidhamu ulikiukwa.
2. Sababu za kuchukuliwa hatua hizo sio sahihi.
Utaratibu ambao unatakiwa kufuatwa kabla ya kumchukulia
hatua za kinidhamu kiongozi kwa mujibu wa Katiba na Kanuni
za Uendeshaji ni kama ifuatavyo;
Kanuni ya Uendeshaji 6.5.6 inasema;
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 2
Kiongozi yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila
kwanza kupewa mashitaka yake kwa maandishi na mamlaka
husika na kupewa nafasi ya kujibu mashitaka kwa maandishi.
Pia tunapenda ijulikane kwamba Kanuni ya Uendeshaji 6.5.2
(a), (b), (c) na (d) kama ilivyorekebiswa Januari 2013 inasema;
Kwa mujibu wa ibara ya 5.4.3 na 5.4.4 ya Katiba mwanachama
yeyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu ama kuonywa ama
kuachishwa ama kufukuzwa uanachama bila kwanza;
a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa
majibu katika muda usiopungua wiki mbili.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao
mnamo wiki mbili baada ya kusikilizwa.
d) Kamati Kuu inaweza kuchukua hatua za dharura bila
kuzingatia utaratibu (b), (c) hapo juu kama itaona maslahi
ya Chama kwa ujumla yanaweza kuathiriwa isipokuwa
mwanachama au kiongozi anayelalamikiwa atalazimika
kuitwa kwenye kikao husika.
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 3
Naomba nichkue fursa hii kufafanua kuwa uongozi wa chama
ulifanya mkutano na waandishi mnamo tarehe 26/11/2013 na
kusema kwamba marekebisho haya ya Kanuni ya mwaka 2013
ambayo nimewawekea hapo juu, ndiyo utaratibu waliofuata. Pia
walieleza kuwa sikuwa naifahamu na nilidanganywa kwani Kanuni
ilishabadilishwa. Mabadiliko haya ambayo ni katika kipengele (d)
kuhusu hatua ya dharura iliyochukuliwa na Kamati Kuu haikugusa
kipengele (a) cha Kanuni. Yaani ni kuwa hata kama Kamati kuu
itachukua hatua ya dharura kwa mujibu wa kipengele (d), bado
kipengele (a) ni lazima ifuatwe na inatamka wazi sharti la kiongozi
kupewa mashtaka kwa maandishi na kupewa nafasi ya kujibu kwa
maandishi. Hii ni haki ya msingi kwa kila utawala au uongozi.
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe hakupewa mashtaka yake aliyakuta
ndani ya kikao baada ya kupewa taarifa kwa ujumbe wa simu (text
message au sms).
Kwa uzito wa makosa hayo yaliyosababisha kuvuliwa uongozi na
kwa kuangalia athari zake kwake yeye binafsi na chama kwa
ujumla, Kamati Kuu ilitakiwa kujiridhisha kwamba Kanuni za
Uendeshaji na Katiba zinafuatwa.
Hili linaendana na utaratibu uliotumika kwa Samson Mwigamba
kuvuliwa nyadhifa yake ya uenyekiti wa mkoa. Yeye hakuitwa
kabisa kwenye kikao hicho na ni ukiukwaji wa Kanuni ya Uendeshaji
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 4
6.5.6(d) niliyoisoma hapo juu kwamba lazima kiongozi huyo aitwe
kwenye kikao.
Sababu zilizotumika ingawaje hajapokea taarifa rasmi ya maandishi
kwa mujibu wa Kanuni za Uendeshaji ni kwamba yeye ameshirki
kwenye kuandaa na kusambaza waraka ambao unasemekana ni
mkakati wa ushindi wenye lengo la kupindua uongozi uliopo.
Waraka huo haukumtaja Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kama
muandaaji au msambazaji. Waliouandaa hawajaukana na badala
yake wamesema waziwazi kabisa kwa maneno na maandishi
kwamba Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe HAHUSIKI. Sio sawa
kumuadhibu Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe kwa hisia au tu kwa
sababu ya urafiki wake na watu fulani.
Haya ni mapungufu ambayo kwa bahati nzuri Katiba na Kanuni za
Uendeshaji zinatoa nafasi ya kurekebishwa kwa kutoa nafasi ya
kukata rufaa. Na utaratibu ni huu hapa;
Kwa ufupi, Ibara 6.3.6(d) ya Katiba ya Chama;
“Kiongozi aliyechukuliwa hatua za kinidhamu na mamlaka
yake ya nidhamu anayo haki ya kukata rufaa ngazi ya juu ya
ile mamlaka yake ya nidhamu na uamuzi wa ngazi hiyo
utakuwa wa mwisho”.
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando 5
Ibara 6.3.6(e) ya Katiba ya Chama;
“Rufaa yoyote lazima ifanyike katika muda wa siku thelathini
tangu tarehe ya kupokea rasmi kwa maandishi maamuzi ya
mamlaka iliyotoa adhabu”.
Kanuni za Uendeshaji zinatoa UTARATIBU ambao unatakiwa
ufuatwe ili kiongozi aliyeadhibiwa aweze kutumia HAKI yake ya
kukata rufani kwa maneno haya;
Kanuni ya 6.5.8 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Kiongozi aliyeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi wa
maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kuamua
kukata rufani au la”
Kanuni ya 6.5.9 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufani atatakiwa kufanya
hivyo katika muda wa siku thelathini baada ya kuarifiwa
uamuzi wa adhabu”
Kanuni ya 6.5.10 ya Kanuni za Uendeshaji;
“Baada ya kutoa uamuzi kikao husika kinalazimika kuandaa
taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha ngazi ya
juu. Taarifa hiyo lazima ifike katika muda wa siku kumi na nne
baada ya kikao cha mamuzi”
Taarifa kwa Vyombo vya habari 11/12/2013 Albert Msando

No comments:

Post a Comment