Saturday, September 1, 2012

UNAZIJUA ...AHADI KUMI ZA MWANA TANU!…



TANU ni chama kilichotuletea ukombozi kutoka kwa wakoloni na kila mtanganyika aliipenda Siasa hii chini ya uongozi wa mwalimu Julius Nyerere kwani ilijali utu, ilikuwa ikiwainua wanyonge na ililenga kulijenga Taifa katika misingi ya usawa, na ulipotakiwa kujiunga na chama hizi ndizo ahadi kumi ulizotakiwa kuziahidi ili utakapotenda kinyume cha hapo uchukuliwe Hatua
Ahadi kumi za mwana tanu zilikuwa kama ifuatavyo.

i. Binadamu wote ni ndugu zangu na Dunia ni moja
ii. Nitaitumikia nchi yangu na binadamu wenzangu wote kwa unyenyekevu na moyo wa upendo na huruma
iii. Nitajitolea nafsi yangu kuondoa umaskini, ujinga, maradhi, na dhuluma hapa nchini na duniani pote.
iv. Rushwa ni adui wa haki, sitatatoa wala kupokea Rushwa.
v. Cheo ni dhamana . sitakitumia cheo changu wala cha mtu mwingine kwa faida yangu.
vi. Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
vii. Nitashirikiana na wenzangu wote kuijenga nchi yetu na dunia yenye haki na amani.
viii. Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
ix. Nitakuwa raia mwema wa Tanzania, Afrika na Dunia nzima.
x. Nitakuwa mtii kwa Raisi na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Ulitakiwa kuapa hivyo unapojiunga na chama, hali hii ilipelekea watu hawa kuwa na uzalendo wa kweli walilipenda Taifa na walijitolea kwa dhati kulitumikia, swali la kujiuliza ni hili kuwa ni commitment gani tunayoiweka tunapojiunga na vyama vya siasa leo!!!
Itaendelea
Kwa makala na mafundisho mabali mabali
tembelea ukurasa wetu wa ujulikanao kama . Changing Youth Changing Nation
Mwl.Tuntufye Mwakyembe

No comments:

Post a Comment