Saturday, September 15, 2012

CHADEMA kuwashitaki RPC, Morogoro, Iringa

Msimamo wa CHADEMA
Wakati hayo yakijiri, CHADEMA kwa upande wake, kimetoa msimamo wa kukataa kwanza, kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nchimbi kuchunguza mauaji ya Mwangosi huko Iringa, lakini pia kinakusudia kuwafungulia mashitaka ya mauaji makanda wa polisi wa mikoa ya Morogoro na Iringa.
Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari jana mjini Morogoro, Ofisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene aliongeza kufikishwa mahakamani kwa askari mmoja anayetuhumiwa kumuua Mwangosi hakuwezi kumaliza kiu ya wapenda haki, akidai kuwa watuhumiwa wengine bado wanatamba mitaani.
“Uamuzi wa Kamati Kuu iliyokaa karibuni ni kwamba RPC wa Iringa, Michael Kamuhanda akamatwe na afikishwe mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya Mwangosi, kwa sababu yeye ndiye alikuwa akiongoza operesheni wakati polisi wanafanya mauaji hayo, alikuwa field.
“Lakini pia CHADEMA tunasema maaskari wote wanaoonekana kwenye picha wakati Mwangosi anakamatwa, kupigwa na kuuwawa ni watuhumiwa wanapaswa kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa mauaji, chini ya hapo ni kuwahadaa wapenda haki Tanzania na duniani kote ambao sasa wanaanza kuiangalia Tanzania kwa jicho la aina yake kutokana na mauaji yanayofanya na vyombo vya dola,” alisema Makene.

No comments:

Post a Comment