Wednesday, September 19, 2012

Rais Obama amkaba Romney kwa ubaguzi

Rais wa Marekani Barack Obama amemshtumu mpinzani wake wa chama cha Republican, katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba Mitt Romney, kwa kubagua sehemu kubwa ya raia wa Marekani.
Bwana Romney alinaswa kisiri na makachero wa Obama kwenye mkanda wa video akitoa matamshi ya kuwadharau baaadhi ya wapiga kura wakati wa hafla ya faragha ya kuchangisha pesa za kampeni katika chama cha Republican.
Akizungumza kwenye mahojiano na kipindi kimoja cha televisheni nchini Marekani Obama amesema jambo ambalo amejifunza akiwa rais ni kuwatumikia wamarekani wote.
Baada ya kuchaguliwa , alisema , atajitahidi kuwahudumia hata wale ambao hawakumpigia kura.

No comments:

Post a Comment