Wednesday, September 26, 2012

Yale ya ccm na chadema ndo haya ya malema na chama chake leo wadai -Malema ana kesi ya kujibu


Julius Melama akiwahutubia wafanyakazi wa migodi waliokuwa wanagoma
Mwanasiasa mwenye utata wa Afrika Kusini Julius Malema amefikishwa mahakamani akikabiliwa na shtaka la kuhaulisha pesa au kujipatia pesa haramu, huku mamia ya wafuasi wake wakikusanyika nje ya mahakama kumuunga mkono.
Ingawa mahakama ilimwachilia kwa dhamana ya randi elfu kumi.
Seng'enge zilizungushwa katika eneo la mahakama hiyo iliyopo Polokwane, mji mkubwa wa jimbo analotokea mwanasiasa huyo,Limpopo.
Malema pia anatuhumiwa kwa kutumia vibaya wadhifa aliokuwa nao kama mkuu wa chama tawala cha African National Congress (ANC) tawi la vijana.
Wafuasi wake wanasema mashtaka hayo yameshinikizwa kisiasa.
Wakiimba na kucheza nje ya mahakama hiyo wafuasi wengi wa chama hicho cha ANC tawi la vijana walishikilia mabango yaliosema 'Muacheni kiongozi wetu'.
Kuna maafisa wengi wa usalama lakini hali ni tulivu.
Julius Malema na washirika wake wa kibiashara wanashutumiwa kwa kufaidi kutokanana na mikataba ya serikali katika jimbo la Limpopo, tuhuma ambazo anazikana. Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 31 pia anachunguzwa katika kesi tofauti ya ukwepaji kulipa ushuru.
Malema ni maarufu sana Afrika kusini kwa ukakamavu wake wa kutetea maslahi ya wananchi na maisha yake ya kifahari, huku akijitambulisha kama mpiganiaji uhuru wa uchumi.
Alitimuliwa kwenye chama hicho tawala mnamo mwezi Aprili akishutumiwa kwa kuzusha migawanyiko katika chama hicho.
Ni mkosoaji mkali wa a Jacob Zuma, hivi karibuni akimshutumu rais huyo kwa alivyoushughulikia mgomo wa wachimba migodi wa Marikana.
Kwa mujibu wa mwandishi wa masuala ya Afrika, Andrew Harding, baadhi ya watu Afrika kusini wanaamini anafikishwa haraka mahakamani, ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kutolewa waranti ya kukamatwa kwake, ili kuimarisha nafasi ya kisiasa ya Zuma.
Mwandishi wetu anaeleza kwamba huenda ikawa ni kesi ya muda mrefu, ambayo huenda ikatoa nafasi ya kujulikana ukweli kuhusu suala hilo la rushwa, ambalo watu wengi wanaamini inaitia nchi hiyo doa.

No comments:

Post a Comment