Thursday, September 20, 2012

TAARIFA KWA WANAROMBO WOTE POPOTE PALE WALIPO DUNIANI HII INAWAHUSU SANA PLEASE SHOW UP!!

Jimbo la Rombo limekuwa na wawekezaji wa ndani na nje pamoja na wafanyabiashara wakubwa na wadogo lakini wamekuwa wakiwekeza nje ya Jimbo na hivyo tatizo la Ajira kwa vijana wa Rombo limeendelea kukua kila siku. Kama nilivyoahidi mwaka 2010 kwenye kampeni tayari wawekezaji wameanza kurudi kuwekeza Rombo na wengine watarudi kuwekeza Rombo.
Mfano ni kiwanda cha Juice na Maji Safi cha SEQUA ambacho kimeanza na uzalishaji wa Maji ya kunywa na Juice zitaanza kutengenezwa hivi karibuni. Lengo ni kuwapa vijana Ajira pamoja na kukuza pato la wakulima wa Matunda. Nitoe Wito kwa wana-Rombo kuanza kulima matunda ya aina mbalimbali kwa wingi ili waweze kukidhi makitaji ya kiwanda hicho ambapo kila siku yatahitajika matunda kati ya tani 5-10.
Pili jana nimezindua kiwanda cha mikate kinachomilikiwa na Tumaini Center ambapo kina uwezo wa kuzalisha mikate 250 kwa saa moja. Tumaini Center ni kituo cha kuwasaidia watoto Yatima kupata Elimu na kwa sasa kina watoto zaidi ya 350 ambapo wapo kwenye level mbalimbali za Elimu kuanzia Primary hadi Chuo kikuu. Nimewaahidi 5million kutoka kwenye CDCF ili ziweze kuwasaidia japo wanafunzi kadhaa kupata elimu hiyo kwa kuwa kituo hiki kimekuwa kikijiendesha kwa miradi yao midogo midogo. Natoa wito kwa Wana-Rombo popote walipo kukisaidia kituo hiki kwa hali na mali ili kiweze kuendelea kutekeleza majukumu yake mazuri kwa ustawi wa Jamii yetu. Kwa wale wasiojua namna ya kukichangia naomba tuwasiliane kwa maelekezo zaidi.

Haya yote nitayasisitiza kwenye Mikutano yangu ya M4C nitakayoianzisha leo tarehe 20-09-2012 hapa Rombo na kumalizika tarehe 2-10-2012.
Leo nitaanzia kata ya Najarareha ambapo pamoja na mambo mengine nitazindua matawi na ofisi kadhaa za Chama wilayani hapa.

Ahsanteni, M4C.
Joseph R. Selasini
Mb.Rombo (CHADEMA)

No comments:

Post a Comment