Monday, September 17, 2012

David Silva atia saini mkataba wa miaka 5

David Silva
David silver
David Silva ametia saini mkataba mpya wa miaka mitano kuendelea kucheza soka katika klabu ya Manchester City, na atasalia katika uwanja wa Etihad angalau hadi mwaka 2017. 
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, mwenye umri wa miaka 26, alijiunga na timu hiyo kutoka Valencia mwaka 2010, na alishindwa kucheza katika mechi mbili tu tangu alipojiunga na City, ambao waliibuka mabingwa wa ligi kuu ya Premier msimu uliopita, na ukiwa ndio ushindi wao wa kwanza tangu mwaka 1968. 
Mchezaji huyo alikuwa amehusishwa na gumzo kwamba alikuwa na mipango ya kurudi Uhispania, lakini amesisitiza atakuwa radhi kuendelea kucheza soka nchini Uingereza."Ninajihisi nimo katika hali ya furaha katika klabu, na hayo ikiwa ni pamoja na wakazi wa mji huyo," ameelezea kupitia tovuti ya club yao leo hii

No comments:

Post a Comment