Friday, September 21, 2012

Je Malema ndiye Mugabe wa Afrika Kusini? au Tumfananishe na nani hapa Tanzania?Nahisi ni Jasiri kama Godbless Lema Wa Arusha mjini.

Julius Malema
Julius Malema
Wakosoaji wa Malema wanamuona kama mhemshaji. Wanasema kiongozi huyo wa zamani wa vijana analenga kutumia mauaji ya Marikana ambayo ndiyo mabaya zaidi kuwahi kufanywa na polisi tangu enzi ya ubaguzi wa rangi miaka 18 iliyopiya kuweza kujinufaisha kisiasa.
Malema anatumai kuwa chama tawala ANC, kitamuondoa rais Jacob Zuma kama kiongozi wake kwenye mkutano wa kitaifa wa chama hicho mwezi Disemba mwakani na hata kubatilisha uamuzi waliochukua wa kumfukuza kutoka kwa chama hicho.
Tangu polisi kuwaua wachimba migodi 34 wa Marikana waliokuwa wanagoma tarehe kumi na sita mwezi jana, Bwana Malema amekuwa akizuru migodi ya Afrika Kusini akiwahutubia wachimba migodi, akiwashauri kutatiza kabisa shughuli katika migodi hiyo.
Mnamo Jumanne, aliitisha mgomo wa kitaifa na na kuwataka wachimba migozi kusitisha uzalishaji wa madini katika mojawapo ya migodi mikubwa ya dhahabu na madini ya platinum.
Kwa mujibu wa mdadisi wa maswala ya kisiasa William Gumede, Malema anatumia mauaji ya Marikana kujinufaisha kisiasa ili aonekane kama mkombozi wa waafrika weusi nchini humo ambao wamezongwa na umaskini. Lakini bwana huyu ana uungwaji mkono wa wafanyabiashara mashuhuri weusi.
Yeye hutembea bila hofu, katika maeneo ya vitongoji duni kabla ya kutoweka katika maeneo ya kifahari.
"ni vigumu kumfungia Malema njia zake. Yeye hutumia lugha safi ya kuwashawishi watu anaowalenga.''anasema bwana Gumede.
Gumede anamfananisha Malema na wanasiasa wa chama tawala nchini Zimbabwe Zanu-PF, kinachoongozwa na rais Robert Mugabe.
"wao hutoa matamshi makali kuhusu maswala ya kijamii.Inapokuja kwa swala la uchumi , wao hutumia matamshi ya ujamaa wakati kimsingi wao ni mabepari ambao hutumia serikali kujibinafsisha maslahi yao,'' anasema Gumede.
'Hafai hata kwa demokrasia'
Tangu mauaji ya wafanyakazi wa mgodi wa Marikana unaomilikiwa na kampuni ya Lonmin, ambayo ipo katika masoko ya hisa ya London na Johannesburg, Malema amepiga jeki, wito wake wa kutaka migodi kutaifishwa.
"waingiereza wanapata pesa nyingi sana kutoka kwa mgodi huu.Sio waingereza waliouawa. Ni ndugu zetu waafrika,'' alitoa matamshi hayo ambayo yanafanana na kauli ambayo hutolewa sana na chama cha Zanu-PF nchini Zimbabwe.
Pia alimfananisha afisaa mkuu mtendaji wa kampuni ya Lonmin Cyril Ramaphosa ambaye ana ushawishi mkubwa katika chama cha ANC, kama kikaragosi cha wazungu na wageni nchini humo.
Raia wengi wa Afrika Kusini wameonekana kughadhabishwa na serikali.
"kila mgodi una mwanasiasa ndani yake. Wao hupewa pesa kila mwezi, pesa wanazoziita hisa. Lakini ni malipo ya kutoa ulinzi kwa wazungu dhidi ya wafanyakazi weusi.'' Malema alidai
Bwana Gumede anasema matamshi kama hayo yanasikizwa sana na wananchi wengi maskini.
Kuhusu matamshi ya bwana Malema kwa mchimba migodi anayeishi katika vitongoji, ni ya kweli. Wakati akizungumzia uzalendo, wanapata matumaini ya kunufaika na utajiri wa madini nchini Afrika Kusini.
Malema anasemekana kutoa wito wa uzalengo kwa niaba ya wafanyabiashara katika jamii ya waafrika kusini weusi.
"wengi wa wafanyabiashara hao weusi walichukua mikopo kununua migodi kwa hivyo wana madeni chungu nzima. Ikiwa migodi itataifishwa itakuwa afueni kubwa kwao," anasema Gumede.
Malema pia ametumia mzozo huu kushinikiza wito wa kutaka rais Jacob Zuma ajiuzulu, akiwaongoza wachimba migodi, katika wito wao wa ''tumechoka na Zuma''.
'' Leo tunaishi maisha mabaya zaidi hata kuliko wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi. Tunauawa na watu wetu. Tunakandamizwa na serikali yetu,'' alisema Malema.
Lakini chama tawala kimemtaka Malema akome kutumia mauaji ya Marikana kujitafutia umaarufu.
Wadadisi wanasema kuwa Robert Mugabe huzua mchanganyiko wa maoni nchini Afrika Kusini. Wengi wanamuona kama mwenye kiburi na anayeamini kuwa utawala unapaswa kuwa wake peke yake.
Kitu muhimu kumhusu Malema ni kwamba, wakati kuna maandamano yanayohusu umaskini yeye huwa hakosekani pale. Kwa hivyo yeye hujaza penzo ambalo viongozi wamekosa kujaza. Na hivyo ndivyo anasalia kuwa vinywani mwa wengi.

No comments:

Post a Comment