Rais wa Marekani Barack Obama amewaomba wakenya ambako babake alizaliwa kujiepusha na ghasia pamoja na vitisho katika uchaguzi mkuu unaokuja.
Uchaguzi mkuu wa Kenya uliokumbwa na utata mwaka 2007 ulisababisha ghasia na vurugu ambapo watu zaidi ya 1,000 waliuawa
Wakenya watapiga kura tarehe 4 mwezi Machi, kumchagua rais na waakilishi wengine, katika uchaguzi mkuu wa kwanza tangu ule uliokumbwa na ghasia.
''Wakenya lazima wakatae vitisho, na ghasia na waweze kuruhusu uchaguzi huru na wa haki. Wakenya lazima wasuluhishe mizozo kwa kupitia mahakamani wala sio kupitia vurugu barabarani,'' alisema Obama
''Lakini cha muhimu ni kuwa wananchi wa Kenya lazima waungane kabla na baada ya uchaguzi kushirikiana kuijenga nchi,'' aliongeza Obama
Babake Obama alizaliwa Kenya na nyanyake wa kambo, angali anaishi katikla kijiji cha Kogelo.
Babake Obama alifariki katika ajali ya barabarabni mwaka 1982.
No comments:
Post a Comment