Mabingwa watetezi wa kombe hilo
Manchester City wameandikisha ushindi mkubwa dhidi ya mabingwa wa ulaya
Chelsea na hivyo kufufua matumaini yao ya kuhifadhi kombe hilo kwa mwaka
wa pili, licha ya kukabiliwa na upinzani mkali kutoka wa vinara wa ligi
hiyo kwa sasa Manchester United.
Mechi hiyo iliyokuwa na mashambulizi na kila
aina ya vivutio baina ya timu hizo zinazomilikiwa na matajiri wawili
tofauti,imemalizika kwa ushindi wa Man City wa mabao mawili kwa bila.Mabao ya kipindi cha pili ya Yaya Toure na Carlos Tevez yalitosha kuizamisha Chelsea, na kufufua matumaini ya Man City, kutetea taji lao ambalo sasa linaonekana kuwa mikononi mwa majirani zao Manchster United wanaoongoza ligi wakiwa na tofauti ya point 12.
Mapema kipindi cha pili, Chelsea, walipata penat baada ya Demba BA, kuangushwa katika eneo la hatari na mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, lakini penat iliyopigwa na nahodha wa Chelsea, Frank Lampard, ilipanguliwa Joe Hart na kuamsha mashambulizi zaidi ya Manchester City.
Kwingineko,katika mchezo mwingine wa leo, Newcastle wakiwa nyumbani,walitoka nyuma baada ya kufungwa bao la mapema na kuchomoza na ushindi wa mabao manne kwa mawili dhidi ya Southampton.
Mabao wa Newcastle yamefungwa na Musa Sisoko,Papis Demba Cisse,Yohan Cabaye aliyefungwa kwa mkwaju wa penati huku bao la nne watakatifu au Southampton wakijifunga.
Mabao ya Southampton yalifungwa na Morgan Scheneiderlin dakika tatu tu baada ya mchezo kuanza huku bao la pili likifungwa na Rickie Lambert.
No comments:
Post a Comment