Sunday, February 24, 2013

Man United yaelekea kushinda ligi kuu



Ligi kuu ya soka nchini England, imeendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbali mbali.
Ryan Giggs
Huko Loftous Road, Manchester United imeebuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya QPR, huku mshambuliaji Ryan Giggs akifunga bao la pili na kufikisha mabao 999 toka aanze kucheza soka la ushindani na kuifanya timu yake ya Manchester United, kuongeza tofauti ya point 15 na mabingwa watetezi Manchester City.
United ilipata bao lake la mapema kupitia kwa Rafael Da Silva ambaye alifunga kwa shuti kali dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza baada ya mlinda mlango wa QPR,Julio Cesar kuokoa kiki la Robin Van Persie.
Rafael ambaye mdogo wake,Fabio yupo QPR kwa mkopo,hii leo alionekana kuwa kwenye kiwango kizuri na kuokoa hatari kadhaa langoni mwa United hasa baada ya kuokoa mpira wa kichwa wa Criss Samba ambao ulikuwa uingie nyavuni.
Licha ya Dan Welbeck na Wayne Rooney kuingia wakitokea benchi,hii leo hawakuweza kupata bao katika ushindi huo ambao unawabakisha United kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka nchini England.
Matokeo haya,yanaendelea kuwabakisha QPR kwenye nafasi ya mwisho ya msimamo wa ligi hiyo yenye upinzani mkubwa duniani.

No comments:

Post a Comment