Maandamano makubwa yalifanywa India kupinga vitendo vya dhulma dhidi ya wanawake

Shirika la kutetea haki za
kibinadamu la Human Rights Watch, limesema kuwa serikali ya India
imekosa kabisa kuwalinda watoto kutokana na dhulma za kimapenzi ambazo
zinatendeka sana katika shule na taasisi za kuwatunza watoto.
Kwa mujibu wa shirika hilo, zaidi ya visa elfu
saba vya ubakaji wa watoto huripotiwa kila mwaka , ingawa wataalamu
wanaamini kuwa idadi kamili huenda ikawa juu kuliko inavyokadiriwa.
Watoto wanaoathiriwa na vitendo hivyo, mara kwa mara huteswa na kunyanyaswa na polisi.
Human Rights Watch limeitaka serikali kutilia
mkazo sheria zilizopo na hata kufanyia mageuzi mfumo wa sheria ili
kukabiliana na hali hii.

Ripoti hii inakuja wakati kuna kilio kikubwa
kutoka kwa watu India hasa kuhusu ubakaji wa msichana wa chuo kikuu
uliofanywa na wanaume watano na kusababisha kifo chake Disemba mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment