Saturday, February 2, 2013

Chelsea yalemewa na Newcastle


Chelsea ikicheza na Newcastle
Moussa Sissoko, alifunga mara mbili kwa ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuichezea Newcastle, ambayo ilikuwa nyuma kwa magoli mawili na kuibuka washindi kwa kuilaza Chelsea.
Mchezaji wa zamani wa Newcastle Demba Ba ambaye anachezea Chelsea alipata nafasi ya kwanza kulishambulia lango la Newcastle.
Dakika chache baadaye, Jonas Gutierrez alifunga goli lakini Chelsea ilijibu mapigo kwa kufunga kupitia kwa Frank Lampard na Juan Mata.
Wachezaji wa Chelsea
Sissoko alisawazisha katika dakika ya 68 na kufunga bao lingine na la ushindi katika dakika za majeruhi za mchezo.
Ilikuwa ni makaribisho mazuri kwa mashabiki wa Newcastle kwa ushindi huo uliochochewa na mchezaji kiungo huyo kutoka Ufaransa, ambaye alitia saini kuichezea Newcastle tarehe 25 mwaka huu.
Kocha wa Newcastle Alan Pardew ameelezea usajili wake mpya wa mchezaji Demba Ba mwenye umri wa miaka 23 kuwa ni mafanikio makubwa kwa timu yake.
chanzo bbc.com

No comments:

Post a Comment