Marekani inatumia ndege za
ujasusi zisokuwa na rubani kuwasaidia wanajeshi wa Ufaransa na Umoja wa
Afrika kupigana na wapiganaji wa Kiislamu wa Mali.
Hatua hiyo inafuatia juhudi za Marekani za kupambana na wapiganaji wenye uhusiano na Al Qaeda kaskazini na magharibi mwa Afrika.
Chad inasema kuwa wanajeshi wake wamekuwa wakipambana vikali na wapiganaji katika eneo la milima kaskazini mwa Mali.
Inaarifiwa kuwa wapiganaji kama 65 na wanajeshi 13 wa Chad wameuwawa.
No comments:
Post a Comment