WAKATI nchini Zimbabwe wanawake wakitumia pampers kukuza ukubwa
wa makalio yao, nchini Marekani wamekuwa wakitengeneza pampers za
cocaine, ambazo huvaliwa na kusafirisha dawa hizo nchi mbalimbali pasipo
kugundulika.
Mbinu hiyo mpya imedaiwa kuwagharimu muda mrefu
waandaaji kutengeneza pampers hizo na baada ya kukamilika huvaliwa
kitaalamu nje ya nguo zao za ndani na huvalia suruali au baibui tayari
kwa kuanza safari.
Maofisa wa forodha kwenye Uwanja wa Ndege wa JFK
wamegundua mbinu hiyo mpya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kuwatia
mbaroni wanawake wawili kutoka Bronx wakiwa wamevalia madawa hayo.
Wanawake hao wamekamatwa na kilogramu 6.5 za dawa
za kulevya aina ya cocaine ambazo walikuwa wamezivalia kwa mtindo wa
nepi nje ya nguo zao za ndani.
Kwa mujibu wa Gazeti la Dailymail la Uingereza,
wanawake hao waliokamatwa baada ya kushuka katika ndege ya JetBlue
iliyotoka Jamhuri ya Dominika huko Santo Domingo ni Priscilla Pena na
Michelle Blassingale, walikamatwa wakiwa na cocaine hizo zikiwa katika
mwonekano wake wa asili.
Kukamatwa kwa pea hiyo ya wanawake, kulitokana na
walinzi kushangazwa na hali ya mbwa waliokuwa nao kuwafuatilia zaidi
wanawake hao na kuanza kufoka ilhali walikuwa hawana mizigo, jambo
lililowasukuma maofisa hao kuamua kuwakagua vilivyo.
Baada ya kuchunguza kwa makini katika mizigo yao,
hawakuweza kuona madawa yoyote, lakini walipojaribu kuwavua nguo zao
walikutana na idadi kubwa ya dawa za cocaine yaliyokuwa yamefungwa
mithili ya pampers nyuma ya makalio yao. Baada ya kugundulika na madawa
hayo haramu, wanawake hao walikamatwa na kupelekwa chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa Dailymail, Blassingale amewekwa
rumande huku akisubiri kufikishwa mahakamani na Pena ameachiliwa kwa
dhamana ya Dola 150,000 (sawa na Sh240 milioni). Mwezi Oktoba mwaka
jana, jasusi wa dawa za kulevya alihukumiwa kifungo cha miaka 300 jela
baada ya kugeuza ndege ya American Airlines kuwa chombo kikubwa cha
kusafirishia dawa hizo.
Victor Baurne (37) aliyekuwa meneja mizigo wa
ndege hiyo alikamatwa katika kituo hicho hicho cha (JFK) John F. Kennedy
International Airport kwa kosa la kusafirisha dawa za thamani zaidi ya
Pauni 330 za cocaine toka mwaka 2000 mpaka mwaka 2009.
Uchawi watumika kikamilisha malengo
Baurne alidaiwa kuwa kwa kipindi chote cha miaka
tisa, alikuwa akisafiri mpaka Afrika kwa ajili ya kudidimiza mwonekano
wowote wa kazi yake ya kusafirisha dawa hizo.
Wakati wa kesi yake, Baurne alikuwa akisafiri mara
kwa mara mpaka Afrika kwa ajili ya kudidimiza kesi yake kwa uchawi,
ambapo alikutana na waganga kadhaa ambao waliweka laana juu ya waendesha
mashtaka, kulingana na nyaraka za mahakama.
chanzo-Mwananchi.
chanzo-Mwananchi.
No comments:
Post a Comment