RAIS wa Zimbabwe Robert Mugabe ametangaza kushiriki kwa mara ya sita kwenye uchaguzi wa urais utakaofanyika nchini humo.
Mugabe alisema hayo wakati wa sherehe ya kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwake ambapo alitimiza miaka 89.
Katika hafla hiyo kiongozi huyo alisema kuwa,
kumekuwa na hila pamoja na shinikizo mbalimbali kutoka Marekani na
Uingereza kwa lengo la kumwondoa madarakani yeye pamoja na chama chake
cha Zanu PF.
Mugabe ambaye anaiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya
miaka 33 sasa amepanga kufanya sherehe kubwa zaidi ya kuzaliwa kwake
mwezi ujao itakayogharimu kiasi cha Dola 600,000.
Wakati Rais Mugabe akijiandaa kufanya sherehe
mwezi ujao, Waziri wa Fedha wa nchi hiyo Tendai Biti alitangaza kuwa,
nchi hiyo imebakiwa na hazina ya Dola 300 kwenye Serikali ya nchi hiyo.
Zimbabwe licha ya kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi, inatuhumiwa kwa hali mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Zimbabwe licha ya kukabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi, inatuhumiwa kwa hali mbaya ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Awamu ya tano ya uchaguzi wa Rais nchini humo
uligubikwa na ghasia pamoja na vurugu zilizosababisha Chama cha Zanu PF
na kile cha MDC kinachoongozwa na Morgan Tsvangirai kuunda Serikali ya
umoja wa kitaifa nchini humo.
Mwanzoni mwa mwezi huu Waziri wa Masuala ya
Kikatiba Eric Matinenga alisema kura ya uamuzi kuhusu Katiba Mpya
itafanyika mwezi Machi.
Serikali hiyo ambayo imefilisika imeomba Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuisaidia kupata Sh21.48 bilioni
kuendesha kura hiyo pamoja na uchaguzi.
“Nilipata ujumbe kutoka kwa Ofisi ya Rais kwamba
tarehe ya kura ya uamuzi tayari imeafikiwa. Kura hiyo itafanyika Machi
16,” Matinenga aliwaambia wanahabari mjini Harare.
Katiba ya sasa ya taifa hilo la Kusini mwa Afrika,
ambayo imefanyiwa marekebisho mara 19, ilianza kutumika baada ya
Zimbabwe kujipatia uhuru kutoka kwa Uingereza mnamo 1980.
No comments:
Post a Comment