Sunday, February 24, 2013

Makubaliano ya mapatano DRC yatiwa saini


Mpiganaji akitembea Rutshuru, kaskazini ya Goma, jimbo la KIvu Kaskazini
Viongozi wa nchi za Maziwa Makuu wametia saini makubaliano ya kumaliza mapigano katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Umoja wa Mataifa umekuwa mpatanishi katika makubaliano hayo ambayo yamekusudiwa kumaliza vita baina ya wapiganaji na serikali mashariki mwa Congo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, alisema anatumai kuwa makubaliano hayo yanayoitwa "mwongozo wa amani na ushirikiano" yataleta amani na utulivu katika eneo hilo.
Lakini piya alisema unahitaji kushughulikiwa kwa muda.
Na piya kuna swala la vipi utatekelezwa.
Makubaliano hayo yakitarajiwa kutiwa saini mwezi uliopita wakati viongozi wa nchi za Umoja wa Afrika walipokutana mjini Addis Ababa.
Makubaliano yanalenga mapatano ya jumla ya kisiasa.
Piya kuna mazungumzo mengine yanayofanywa nchini Uganda baina ya wapiganaji wa kundi la M23 na wakuu wa serikali ya Congo.
Pande hizo zimekuwa zikizozana juu ya udhibiti wa eneo la Kivu Kaskazini lenye utajiri wa madini.
Haya ndio mapigano ya karibuni kabisa katika mizozo ya Congo iliyoendelea kwa karibu miongo miwili.

No comments:

Post a Comment