Maelezo yaliyotolewa na James
Samwel wa kikosi cha zimamoto Ultimate Security ni kwamba wao walipata
alarm ya moto na walikwenda eneo la tukio na kukuta moshi unatoka mkubwa
sana kwenye gorofa ya 19, kulikua na watu wanne gorofa ya 19 na wawili
gorofa ya 16 ambao hao waliokolewa mwanzoni, moto ulipozidi uliongeza
moshi zaidi hivyo kazi ya kuwaokoa wanne walioko juu ilikua ngumu lakini
baadae waliokolewa.
Bado haijajulikana ni kiasi
gani cha mali kilichoharibika lakini James anasema hakuna uharibifu
mkubwa sana, ni baadhi ya vitu tu vimeharibika ambapo chanzo cha moto ni
hitilafu ya umeme uliokua ukikatika na kurudi, hakuna yeyote
aliyejeruhiwa ambapo watu sita waliokuwemo eneo la tukio wote waliokolewa salama.
James ameiambia millardayo.com
kwamba hizo floor mbili zilizoungua kwa ndani moja wapo inahusika na
kampuni ya mtandao ya Vodacom na floor nyingine hajajua ni ofisi ya
kampuni gani lakini millardayo.com inaendelea kufatilia.
No comments:
Post a Comment