Tuesday, November 26, 2013

Ufaransa yaongeza majeshi A. Kati


 
Majeshi ya Ufaransa yakiwa ndani ya Kifaru cha kijeshi
Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imethibitisha kuwa imetuma mamia ya wanajeshi wa ziada kwenda kusaidia kuimairisha hali ya usalama Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa ya Umoja wa Mataifa umesema hali ya usalama nchini humo ni ya wasi wasi huku ikionya huenda mauaji ya halaiki yanaweza kuendelea.
Ufaransa imekuwa ikitoa msukumo kwa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa ambalo linazungumzia namna ya kuyasaidia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema raia katika eneo la Jamuhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakikumbana na matatizo yaliyozidi uwezo wao ikiwa ni pamoja na unyanyasi wa kijinsia, utesaji, mauaji na fujo kati ya wakristo na waislamu.
Majeshi ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakijaribu kuimarisha hali ya usalama nchini Afrika ya Kati tangu Rais Francois Bozize apinduliwa mwezi Marchi.

No comments:

Post a Comment