Friday, November 15, 2013

BREAKING NEWS.......ZITTO AWAFUNGULIA KESI WANAO MCHAFUA NA KUMTISHIA MAISHA.

Zitto Kabwe akiwa makao makuu ya polisi upelelezi akiandika statement dhidi ya wanaomchafua na kumtishia.
 Mh. Zitto ameyaandika yafuatayo katika ukurasa wake wa Twitter na facebook.
"Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe". Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM. Wahusika waendelee kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani. Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa tuhuma za uongo.
Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa."  alisema zitto.

Tutaendelea kuwahabarisha pindi tutakapo mpata Mh.Zitto kwa maelezo  zaidi.

No comments:

Post a Comment