Wednesday, November 27, 2013

Ratiba ya Uchaguzi ndani ya CHADEMA


Awali, Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo wa Chadema hicho, Benson Kigaila alieleza maazimio ya Kamati Kuu ya chama hicho kuhusu kujipanga kuanzia ngazi ya chini mpaka taifa.
Pia aligusia suala la kugatua madaraka kutoka makao makuu kwenda katika Kanda 10 pamoja na Progamu ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C), ambayo utekelezaji wake ulikuwa na awamu nne unaombatana na mafunzo mbalimbali.

Kuhusu uchaguzi, alisema kuanzia Novemba 22 hadi 14 Desemba, mwaka huu ni kipindi cha kukamilisha usajili wanachama kuanzia ngazi ya chini.
“Tarehe 15 Desemba mpaka 15 Januari, 2014 utafanyika uchaguzi katika ngazi za vitongoji. Kuanzia tarehe 16 Januari  hadi 30 Januari, 2014 kitakuwa kipindi cha kukata rufaa na kukagua ukamilifu wa uchaguzi wa ngazi hiyo,” alisema Kigaila na kuongeza:
“Februari 1 hadi 15 mwaka 2014, utafanyika uchaguzi ngazi za matawi (vijiji kwa vijijini na mitaa kwa mjini), kuanzia Februari 16 hadi 29, itakuwa kipindi cha kukata rufaa na ukaguzi kwa ngazi hiyo.”
Alisema kuwa kuanzia Aprili Mosi hadi 10, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi ya majimbo ya uchaguzi ambayo yapo 236 na kuanzia Aprili 25 mpaka Mei 5, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi ya wilaya.
Alisema kuanzia Mei 20 mpaka 25, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi za mkoa na Juni 6 hadi 9, 2014 utafanyika uchaguzi katika Kanda zote 10 na Juni 23 mpaka 30, 2014 utafanyika uchaguzi ngazi ya taifa.

No comments:

Post a Comment