Friday, November 22, 2013

P-SQUARE waahidi kutoa burudani yenye kiwango kwa watanzania

Embedded image permalink
Mkuu wa vipindi Nasser Kingu akiongea machache kwenye press conference Hyatt Recency            
Kundi la P-SQUARE lililotua jana nchini Tanzania toka Nigeria kwa ajili ya tamasha kubwa litakalofanyika siku ya kesho pale Leaders club wameahidi kutoa burudani yenye kiwango cha juu kwa watanzania wote watakaohudhuria.

Wasanii hao mapacha kesho jukwaani watapiga muziki wa LIVE na bendi kwa masaa mawili mfululizo huku wakipewa shavu na Lady Jay Dee, Professa Jay, Joh Makini na Ben Pol.


Tamasha hilo kubwa la muziki kwa mwaka huu, linatarajiwa kuanza saa 1 jioni bila kuchelewa.

No comments:

Post a Comment