Wednesday, November 20, 2013

Ghana , Algeria zafuzu Kombe la Dunia

Asamoah Gyan mshambuliaji wa Ghana
Ghana na Algeria jumanne zimeungana na timu za Nigeria, Ivory Coast na Cameroon kukamilisha nchi tano zitakazowakilisha bara la Afrika katika fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka 2014.
Ghana wakicheza ugenini dhidi ya Misri pamoja na kufungwa magoli 2 - 1 walifanikiwa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa vile katika mechi ya awali Ghana iliifunga Misri magoli 6 - 1.
Katika mechi hiyo ya marudiano goli la kwanza la Misri lilifungwa na Amr Zaki huku la pili likitiwa kimiani na Gedo.
Ghana walijipatia goli katika dakika za mwisho mwisho lilofungwa na Kevin-Prince Boateng na hivyo kuzima kabisa matumaini ya Misri kushiriki kombe la dunia mwaka kesho.
Hadi mpira umalizika Misri ikawa imeifunga Ghana 2 - 1 japo ushindi huo haukuisaidia kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia.
Kwa upande wake Algeria pamoja na kufungwa katika mechi ya awali na Bukirna Faso 3 - 2 waliweza kuifunga Burkina Faso 1 -0 na kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia kwa kunufaika na magoli mawili ya ugenini.
Goli pekee lililoizamisha Burkina Faso lilifungwa na Madjid Bougherra baada ya kupigwa mpira wa adhabu na kumshinda mlinda mlango ambapo Bakary Kone alijaribu kuokoa bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment