Tuesday, November 12, 2013

SIFA 10 ZA CCM KWA SASA-PETER KISUMO,kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na mjumbe mstaafu wa bodi ya wadhamini

Wiki chache zilizopita, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na mjumbe mstaafu wa bodi ya wadhamini wa chama hicho kikongwe nchini, Peter Kisumo, wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere alipata ujasiri wa ajabu na akatamka sifa za CCM kwa sasa. Kisumo hakusema kwa siri. Aliweka wazi.
Sifa ya kwanza, amesema CCM ni chama dola, maana huingilia hata madaraka ya mihimili mingine, huingilia uendeshaji wa Bunge, huingilia uendeshaji wa mahakama, hivyo hufanya kila liwezekanalo kulazimisha vitu hata kama sio vya kweli, na havina tija.
Sifa ya pili, CCM inakaa mbali na wananchi. Haya sio maneno yangu, ni ya Kisumo. Hivyo chama hicho hakipo kwa maslahi ya wananchi wengi hasa wa hali ya chini. Rejea wimbo wa “Acha waseme Chama Cha Mapinduzi kina wenyewe”, uliotungwa na Kapteni John Komba.
Sifa ya tatu, imeshindwa kudhibiti rushwa, huduma za jamii nchini zimedorora, elimu imekuwa mbovu, kila idara inatawaliwa na rushwa.
Watanzania wanajua, Kisumo amesisitiza tu wakielewe chama hiki kuwa hakiwezi kudhibiti rushwa. Nimeambiwa tumuunge mkono huyu mzee, kuna kitu tunajifunza hapa.
Sifa ya nne, CCM imeshindwa kuwadhibiti hata walarushwa wenyewe. Watanzania wanajua, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, na Mnadhimu wa Upinzani Bungeni walitaja orodha ya mafisadi katika viwanja vya Mwembeyanga Temeke, lakini hadi sasa CCM imeshindwa kuwadhibiti, licha ya kututajia kuwa ina mafisadi watatu.
Sifa ya tano, Kisumo amesema CCM ni ya walalamikaji. Hata Rais na Waziri Mkuu wanalalamika, hawachukui hatua. Watanzania wanajua kuwa waziri wetu mkuu aliwahi kubanwa kwa kauli zake akaamua kulia bungeni. Kama Waziri Mkuu analia na kulalamika bila kuchukua hatua zozote, Watanzania wote wanajua kuwa viongozi wa chama hicho tawala ni walalamikaji.
Sifa ya sita, amesema CCM ni bubu. Bubu maana yake haiwezi kuongea, haina sauti, na bubu mara nyingine hasikii, hivyo Kisumo anamaanisha kuwa chama hicho ni kiziwi, dhana inayoondoa ile nyingine ya kusema ni sikivu. Bubu hata kama akiwa sikivu hasikii sauti. Hii ni sifa nyingine ya CCM.
Sifa ya saba, amesema CCM haiwezi kukemea, maana yake ni kama vile una mbwa ambaye hawezi kubweka, kiziwi, bubu kama inavyobainishwa, hivyo hana tija hawezi kupambana, ni pambo tu.
Sifa ya nane, amesema CCM ina matumizi mabaya ya rasilimali na zinatumiwa na wananchi wachache kwa manufaa yao. Hili linajulikana ndiyo maana viongozi wanalalamika kila mara kuwa pengo kati ya wenye navyo na wasio navyo linaongezeka. Chama hicho ndio vinara.
Sifa ya tisa, CCM haikubaliki kwa wananchi, hata ikishinda katika uchaguzi mkuu ujao haitakuwa na nguvu bungeni, itaangushwa. Haya si maneno yangu ni ya mdhamini wao. Yeye kaona ila najua wengine wanang’ang’ania kusadikisha watu uongo, kama wanavyofanya Nape, Kinana, Mangula, Chikawe, Wassira, Lukuvi, Pindi Chana na wengine.
Sifa ya kumi na ya mwisho, CCM kushindwa uchaguzi mkuu ujao uwezekano ni mkubwa. Huyu kada ameona, ametafakari kwa uzee wake akaona na akaamua kusema.
Kama huo utabiri ni wa kweli, chama mbadala ni CHADEMA ambacho kinaweza kusaidia wananchi kufanya mabadiliko.

No comments:

Post a Comment