Saturday, November 16, 2013

Ni hali ya kusikitisha Ufilipino

Wakaazi wengi bado wangali kupata msaada
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufilipino, ameambia BBC kuwaidadi kamili ya watu waliojeruhiwa kutokana na Kimbunga Haiyan, wiki jana, imefika watu elfu tatu na miatano.
Bwana Mar Roxas amekiri kuwa idadi hiyo hata hivyo huenda ni kubwa zaidi ya hiyo.
Ingawa idadi rasmi ya waliofariki bado haijulikani na maafisa katika moja ya majimbo yaliyoathirika zaidi kuliko yote, wanasema kuwa watu elfu nne wamefariki jimboni humo pekee.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa serikali italazimika sasa kuanz akufanya mipango ya ujenzi mpya na wa kudumu.
Serikali inakadiria uhariobifu uliotolkea kuwa wenye thamani ya dola bilioni 15.
Asilimia tisini ya nyumba zimeharibika na maefi ya shule haziwezi tena kutumika.
Watoto hawaedni tena shule hadi mwezi Januari.
Wakati huohuo, wafanyakazi wa kutoa misaada nchini wametaja hali iliyoko nchini humo kama ya kusikitisha, wiki moja tu baada ya kimbunga haiyan kupiga maeneo ya kati ya nchi hiyo. Maelfu ya raia wa nchi hiyo bado wanahitaji misaada ya dharura.
Msemaji wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka, la Medcins sans Frontiers, Henry Gray, amesema masuala mengi ya mipango yanaathiri shughuli ya kusambaza misaada.
Katibu mkuu wa muungano wa nchi wanachama wa muungano wa asia na pacific ASEAN Lee lair-un min amesema misaada zaidi itatolewa na kuwa mataifa yote duniani yanaweza kufanya mengi zaidi kusaidia.

No comments:

Post a Comment