Sunday, November 10, 2013

Jana nilijaribu fatilia hii ishu ya Skendo ya Zitto.


Katika pita pika nakukatana na Hii kitu.



1. Ile Report ya kuchunguza mwenendo wa Zitto nimejaribu kuusoma ila ukiuelewa utagundua kwamba una chembe chembe za Kupikwa yan sio kweli, japo kuna baadhi ya vitu vinaweza kuwa na uhalisia. Me naziita siasa chafu ambazo hata kwenye Chaguzi kichuo chuo zipo. Wamesema kala mabilioni ya CCM kuihujumu Chadema, bt nashangaa ni Report gani ambayo haina Attached Docs za Transfer au Transaction no au Codes au supportive docs yoyote toka hata Western Union zilizokua zaingia kwa Zito.



2. Nimesoma alichojibu Zitto, simply yani kamuomba Dk. Slaa athibitishe kama ile ni Taarifa rasmi toka Chadema na kakanusha si kweli. Pia kazungumzia uhusishwaji wa Dk. Kimei na Andrea Codes, kwamba wakitaka kumchafua wamchafue yeye lakini wasichafue na Career za watu wengine.



3. Nimebahatika kuona Mail aliyotuma Andrea Codes kwa Chadema ya kuwataka wakanushe taarifa hiyo ambayo yeye ametajwa au kama ni kweli ni ya chadema basi wampe Go ahead ya kuwashtaki kwa kumchafua yeye na Organization yake. Hiyo picho inasemekana ndo alichojibiwa na Mnyika kwamba ile si taarifa ya Chadema, je nani kaitoa?



4. Nimesoma taarifa ile ya Deo ambayo zito anasema ndo ametishiwa maisha na jamaa amesema ni kweli zitto anahusika kuihujumu chadema kwa kushirikiana na Mwigulu na Ridhiwani kwa matukio mbali mbali likiwemo la Arusha.



Hapa naendelea Fatilia any Update nyingine itakayotokea.


Hii Move tamu sana ila siku si nyingi Mnafki atajulikana ni nani.

No comments:

Post a Comment