Saturday, November 16, 2013

Sri Lanka yakataa uchunguzi wa kimataifa

Waziri mmoja wa Sri Lanka amekataa wito wa waziri mkuu wa Uingereza kwamba ufanywe uchunguzi wa kimataifa kuhusu madai ya uhalifu wa kivita uliofanywa mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchi hiyo.
David Cameron kwenye mkutano wa Commonwealth, Sri LankaWaziri wa maendeleo ya kiuchumi, Basil Rajapakse, ndugu wa Rais Mahinda Rajapakse, aliwaambia waandishi wa habari kwamba uchunguzi kama huo kamwe hautoruhusiwa.
Matamshi yake yanafuatia tamko la waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba Uingereza itauomba Umoja wa Mataifa kuanzisha uchunguzi wa kimataifa, iwapo Sri Lanka yenyewe haikuanzisha uchunguzi utaojitegemea ufikapo mwezi wa March.
Bwana Cameron alisema hayo nchini Sri Lanka ambako anahudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola.
Ijumaa Bwana Cameron alikutana na Rais Mahinda Rajapakse.

No comments:

Post a Comment