Monday, September 3, 2012

Wachimba migodi 50 waachiliwa Afrika Kusini

wachimba migodi walioachiliwa
Takriban wachimba migodi 50 wa Afrika Kusini wameachiliwa huru na mahakama moja nchini humo baada ya mahakama hiyo kutupilia mbali mashtaka yote dhidi yao.
Hatua hii inakuja siku moja baada ya wendesha mashtaka kufutilia mbali mashtaka dhidi ya wachimba migodi
270 kufutia shinikizo za uma.
Walifikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji ya wachimba migodi wenzao 34 waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Hapo awali polisi waliwapiga riasasi na kuwajeruhi wachimba migodi wanne katika tukio tofauti .
Inadaiwa kuwa polisi walitumia risasi za mipira kuwatawanya waandamanaji katika Mgodi mwingine wa Gold Miners wanaogoma wakidai nyongeza ya mishahara ndipo wanne hao walipojeruhiwa.
Kisa hiki kinafuatia kuuwawa kwa wachimba migodi wengine 34 wakati walipopigwa risasi na polisi wiki mbili zilizopita.
Mashtaka dhidi ya wachimba migodi waliofikishwa mahakamani, kwa mujibu wa kanuni ya enzi ya ubaguzi wa rangi, yaliakhirishwa kwa muda baada ya malalamiko ya umma.
Wachimba migodi wa kwanza miamoja walitarajiwa kuachiliwa leo wengine wakisubiri kuachiliwa siku ya Alhamisi.
Mazungumzo yanayolenga kusitisha mgomo wa wachimba migodi hao wa mgodi wa madini ya Platinum wa Marikana, vile vile yalitarajiwa kuanza leo.
Polisi wanadai kuwa walilazimika kuwafyatulia risasi wachimba migodi hao kama hatua ya kujilinda kwani na wao walikuwa wamejihami kwa mapanga wakati wakikabiliana nao.
Mgomo wao ulioitishwa kulalamikia nyongeza ya mishahara pamoja na kutaka chama chao kipya cha wafanyakazi kutambuliwa, ungali unaendelea huku mgodi ukisalia kufungwa kwa wiki tatu sasa.
Hata hivyo kampuni inayomiliki mgodi huo, Lonmin, ambayo ndio ya tatu kwa ukubwa wa uzalishaji wa madini hayo, imesema kuwa mgomo huo ni haramu.
Lakini imetupilia mbali matakwa yake kuwa ikiwa wafanyakazi hao hawatarejea kazini , watafutwa kazi.
Baada ya ufyatuliaji risasi, viongozi wa mashtaka wa serikali, walitumia kanuni ya enzi ya ubaguzi wa rangi ya kosa la ujumla kuweza kuwafungulia mashtaka wachimba migodi 270 waliokamatwa wakati wa vurugu baada ya mgomo wao kuwalazimisha polisi kuwafyatulia risasi.
Kanuni hiyo ilitumika na walowezi wa kizungu wakati wa enzi ya ubaguzi wa rangi kuwanyanyasa wapinzani wao waafrika weusi.

No comments:

Post a Comment