Tuesday, September 4, 2012

ULAZIMA WA TOBA JUU YA DAMU ISIYO NA HATIA KUMWAGIKA JUU YA NCHI-Mwakyembe


Inapotokea Damu inamwagika katika Matukio mbalimbali na hasa ile isiyo na hatia kuna mambo kadha wa kadha huambatana na hali hii, hebu tuangalie Baada ya kaini kumuua Abeli Mungu anazungumza nini na kaini katika Mwano 4:10 anasema “Umefanya nini! Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika Ardhi, Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee Damu…”

Nataka tuelewe sifa za Damu, sifa ya kwanza Damu inazungumza: Mungu alisema sauti ya damu ya ndugu yako inanililia…
Sifa ya pili Damu inaweza ikalaumu,ikalaani na hata kudai kisasi ( anaposema sauti ya damu inanililia, maana yake ina laumu, inadai kisasi nk)
Sifa ya tatu Damu ina uhai ( kama inaweza ikalia ikalaumu maana yake ni kuwa ina uhai)
Hivyo basi Damu inapomwagika katika ardhi pasipo hatia huachilia laana ( Mungu alimwambia Kaini Basi sasa umelaaniwa wewe katika ardhi iliyofumbua kinywa chake ipokee damu. Kwa tafsiri nyingine ni kuwa unapomwaga Damu ya mtu laana huachiliwa juu yako maana ile damu itakuwa ikipiga kelele mbele za Mungu ikilalamika, ikidai kisasi maana inasema nimeonewa au tumeonewa, ndio sababu Mungu alitoa amri ya kutokuuwa., sasa ukisoma Mwanzo 9:6 anasema “Atakayemwaga damu ya mwanadamu, damu yake huyo itamwagwa na mwanadamu; maana kwa mfano wake Mungu alimfanya mwanadamu.” Akimaanaisha mwanadamu hatakiwi kumwaga damu ya mwanadamu mwenzie maana laana ya mauti itaachiliwa juu yake nae atakuja kuishia kuuwawa. ukisoma Mith 6:16 utakuta ansema “kuna vitu sita anavyovichukia Bwana naam, viko saba vilivyo chukizo kwake : macho ya kiburi, ulimi wa uongo, na mikono imwagayo damu isiyo na hatia.” Nilitaka uone Mungu anasisitiza usihusike kumwaga damu isiyo na hatia.

Madhara: Damu ikisha mwagika au kwa ajali au kwa mtu kupigwa ile Damu inaanza kulalamika mbona wanao safari ni wengi lakini mimi tu ndie nilyekufa au walioiba ni wengi mimi tu nimemwaga Damu, au mbona wanaohusika na mambo ya siasa ni wengi lakini ni mimi tu ndie niliyeuwawa kikatili, hii ni mifano tu ya Damu nyingi zilizo mwagika na zinazolalamika na kudai kisasi, sasa Damu ikianza kudai kisasi nguvu za giza huwa zinapata mlango wa kutekeleza madai ya hizi Damu, mifano ni hii kuwa eneo ambalo lilitokea ajali mbaya baada ya muda huwa inatokea tena ni kwa sababu kuna damu inadai kisasi kwamba tufe wengi kwani sisi tuliofia hapa tulikuwa tunamakosa gani! Haivyo baada ya mda mfupi unashangaa ajali inatokea tena eneo lilelile.

Hivyo hivyo katika siasa kama kuna damu ilimwagika katika tukio la kisiasa isiyo na hatia itadai kisasi usishangae utakapoona watu wanaendelea kufa hata kama polisi hawatahusika kabisa, utasikia tu wafuasi wa chama hiki walipigana na chama hiki watu kadhaa wakauwawa, kinachotokea ni utendaji wa nguvu za giza katika kulipiza kisasi cha ile Damu iliyowahi kumwagika katika matukio ya aina iyo.

Jambo la kufanya kwa watoto wa Mungu.
Ukisikia au kusoma katika magazeti kwa habari ya Damu iliyomwagika kwenye ardhi ya Tanzania jua damu iyo itakapodai kisasi na mapepo yakaingia katika utendaji, damu zingine nyingi zitaendelea kumwagika, atakayehusika ni mtanzania mwenzako, baba yako, kaka yako, mama yako nk. Jambo pekee linaloweza kuzuia hiki kitu kisitokee na hata kutoendelea kabisa ni maombi ya toba, tubu kwa ajili ya aliyemwaga damu isiyo na hatia, tubu kwa ajili ya ardhi iliyopokea damu, tubu kwa ajili ya iyo damu iliyomwagika, ita Damu ya Yesu ambayo ndiyo master blood inene mema juu ya ardhi na juu ya ile damu iliyomwagika na juu ya aliyemwaga damu, watoto wa Mungu wakifanya hivi mapepo yanakosa mlango wa kufanya utekelezaji juu ya ile damu iliyomwagika jambo litakalosababisha muendelezo wa matukio kama hayo kukatika, na laana iliyokuwa iachiliwe kwenye nchi kuondoka kabisa ukisoma Efeso 1:7 anasema “Katika yeye huyo, kwa Damu yake, tunao ukombozi wetu masamaha ya dhambi sawa sawa na wingi wa Rehema zake”. Amini kuwa damu ya Yesu inamaliza kila kitu.

Najua roho itakuuma sana ungetamani kuona kisasi cha Mungu , usiwe Eliya aliyefunga mvua akasahau kuwa na yeye yumo katika nchi iyo iyo. Maandiko yanasema wazi kisasi ni juu ya Bwana alafu maandiko yanasema msipowasamehe watu maovu yao Baba yangu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi maovu yenu.
Ni wito wangu kwa wa watoto wa Mungu Tanzania kufanya maombi ya toba juu ya Damu zisizo na hatia zilizotokea kumwagika, maandiko yanasema wawili wenu watakapokutanika katika jambo lolote watakaloliomba watafanyiwa na baba yangu aliye mbinguni.

Pliiiz tenga walau dakika kidogo kila siku kufanya maombi ya toba kwa ajili ya nchi.

Mkaribishe na mwingine asome ujumbe huu.
kwa mafundisho na changamoto mbalimbali -0715629562

No comments:

Post a Comment