Sunday, September 2, 2012

SEHEMU YA UMATI WAWATU WANAOTARAJIA KUMZIKA WAZIRIMKUU WA ETHIOPIA MR.MELES ZENAWI.





 
Ethiopia inatarajia kuuzika leo mwili wa kiongozi wake aliyehudumu kama waziri mkuu kwa muda mrefu nchini humo Meles Zenawi katika mazishi ya kitaifa.
Wakuu wa nchi kadhaa za Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo huku tayari wawakilishi kutoka mataifa ya kigeni wakiwasili Ethiopia jumamosi na kutia sahihi zao katika kitabu cha maombolezo.
Raisi wa Rwanda Paul Kagame na Boni Yayi, wa Benin, ni miongoni mwa viongozi wa Afrika waliowasili mapema katika shughuli za mazishi wa Meles Zenawi.
Raisi wa Benin Boni Yayi ameeelezea kifo cha Zenawi kimeacha pengo kubwa sio tu kwa Ethiopia bali kwa kwa bara zima la Afrika kwa sababu ya maono ya kiongozi huyo na kuunga mkono harakati za kutetea uafrika.



Rais Jakaya Kikwete akiweka akitoa heshima mwisho baada ya kuweka shada la maua kwa aliyekuwa Waziri mkuu waa Ethiopia Marehemu Meles Zenawi katika ikulu ya Addis Ababa jana. Picha na Ikulu.



No comments:

Post a Comment