Kuna Kelele nyingi sana juu ya viongozi kusafiri nje ya nchi.Kuna baadhi ya wana-CCM wanajaribu kutumia Safari ya Dr.Slaa nje ya nchi kuhalalisha safari za Kikwete alizofanya nje ya nchi.
Rais Kikwete
amesafiri mara 357 tangu aingie Madarakani kwa kipindi cha miaka 7 na
miezi kadhaa akitumia Kodi za watanzania ambao wanaambiwa kwamba ni
lazima wachangie kodi ya laini za simu hata kama wapo kijijini na
kutumia laini hizo kuwabip watoto wao walioko mjini bila kazi
maalumu.Kodi hizo ni sehemu ya kugharamia safari hizi za Rais kama
nitakavyoonyesha pichani hapo chini.Katika siku 357 alizosafiri,
zimepungua siku 8 tu akamilishe mwaka wenye siku 365. Hapa tumeongelea
safari ya siku moja tu,kuna nyingine amekaa nje zaidi ya wiki na
nyingine wiki 2 kama hii aliyoifanya juzi.Safari nyingine sio Muhimu
hata kidogo.Kuna nyingine zinamhusu waziri wa Mambo ya Nje,nyingine
zinawahusu Mawaziri wa Utalii na hata Wakurugenzi wa Idara.Delegation of
power(Kukasimisha madaraka) haipo katika Utendaji wake.Hata kama Rais
hana Management skills,washauri wake walitakiwa kumshauri na kumwambia
ukweli kuhusu hili.
Sasa hivi dunia ni kama kijiji,ni lazima
tutumie fursa ya teknolojia.Sio Lazima kwa Rais kusafiri na kuwepo
kwenye mkutano physically.Baadhi ya Mikutano hufanyika kupitia
Mitandao.Balozi zetu nje zinaweza kuwa empowered na kuiwakilisha
serikali kwenye mikutano mingine ya uwekezaji.Waziri wa Mambo ya Nje
Bernard Membe mara kadhaa amekua akiongea kama vile ni mtu anayeelewa
sana dhana ya Economic Diplomacy.Sijui ni kwanini hataki kumshauri Rais
Kikwete ambaye nina uhakika hana taaluma ya Diplomasia na Uhusiano wa
kimataifa au hata taaluma yenye uhusiano na fani hiyo ingawa
alijitutumua kisiasa alipokua waziri wa Mambo ya nje.Pamoja na kuwa na
shahada ya Uchumi ya miaka hiyo ya 1970,sidhani kama Rais wetu( kama
ilivyo kawaida ya Waafrika wengi) alifanya jitihada za kuendelea
kujisomea nadharia nyingine au kujiendeleza kitaaluma(hata kwa kozi
fupi) kulingana na mabadiliko ya Dunia ukizingatia kuwa alijiandaa kwa
Miaka 10 kuwa Rais wa nchi(Kama alivyokiri mwenyewe).Diplomasia ya
Uchumi alitakiwa aielewe.Sio busara kujiandaa kwa kujikusanyia mashabiki
bila wewe kujiandaa kitaaluma kulingana na mahitaji ya muda.Ni uzembe
na usalaiti.
Rais wa Zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ndiye
Mtawala aliyeweka Rekodi ya kusafiri mara nyingi zaidi.Viongozi wa
Afrika wakisafiri mara nyingi hutumia gharama kubwa na misafara
mikubwa.Matumizi mabaya ya fedha. Tanzania sasa inabidi kuwe na tume ya
kudhibiti Ziara za Rais maana kama ndani ya Miaka Saba na miezi kadhaa
Rais Kikwete amekaa nchini kwa miaka 6 tu sasa tunaelekea wapi?
Rais amesafiri nje ya nchi kwa wastani wa safari 45 kwa mwaka 1.Ni
wastani wa safari 4 kwa Mwezi 1.Ni wastani wa safari 1 Kila wiki. Katika
siku 5 za kufanya kazi kiofisi(Sheria zetu za kazi ziangaliwe
upya),Rais anasafiri nje ya nchi siku 1.Yaani kuanzia Jumatatu hadi
ijumaa,siku 1 Rais yupo safarini nje ya nchi kwa siku moja.Hapa
hatujajumuisha idadi ya siku anazokaa humo
Waziri wa Mambo ya
nje angesafiri hivyo tungemuelewa lakini kwa sababu za msingi.Aliyekua
waziri wa Mambo ya nje wa Marekani(Taifa lenye Nguvu duniani za kiuchumi
na Kijeshi) Bi.Hillary Rodham Clinton alikua muumini wa Falsafa ya
Msanii wa Brooklyn,Woody Allen kuwa asilimia 80 ya mafanikio ya
makubaliano au kikao chochote muhimu ni Uwepo wako. She reinforced the
power of being there -- in a place, in a context, in a moment. Hillary
aliweka rekodi ya kusafiri masaa 2,084.21 sawa na wastani wa siku 86.83
na jumla alisafiri siku 401.Huyo ni mtu aliyekua waziri wa mambo ya nje
wa Taifa lenye ushawishi duniani kwa maslahi ya Taifa lake huku Rais
akisafiri mara Chache.Alipokuja Tanzania Rais aliacha kazi zote na
kuvuruga itifaki,alienda Kumpokea badala ya Waziri wa mambo ya nje
kuchukua nafasi yake.Delegation of power hapa sijui ilikua in a reverse
order ama ni nini?!
Mwalimu Nyerere katika Miaka 24 ya utawala
wake alisafiri mara 60+ lakini JK kwa mika isiyofika 8 amesafiri karibia
mara 360. Tunaambiwa(Kwa kufuata utamaduni wake ule wa kuambiwa) kuwa
safari moja ni zaidi ya Sh.300,000,000(milioni 300) na pia tukifanya
kuwa kila safari moja kwa kiwango cha chini anakaa siku 3 maana yake ni
(357 X 3) sawa na siku 1071 ambayo ni sawasawa na miaka 2 na miezi 9
,wiki 3,siku 4, masaa 4 na dakika 3, na sekunde 30 nukta 3.Huyu ndiyo
Rais wa nchi ambayo ni miongoni mwa nchi Maskini duniani ambaye zaidi ya
asilimia 50 ya Raia wake wanaishi chini ya dola moja ya Marekani kwa
siku yaani zaidi ya nusu ya watanzania milioni 45 ambayo ni sawa na watu
milioni 22.5(22,500,000) hawawezi kumudu matumizi ya Shilingi 16,00/
kuanzia saa 12 alfajiri hadi saa 12 alfajiri ya siku inayofuata.Rais
Hajui ni kwani hali hii imekua hivi,hata yeye anashangaa.Hata hivyo ili
kufidia nakisi ya bajeti(deficit) ya shilingi bilioni 264,inabidi Raia
hawa hawa watozwe kodi ya laini za Simu kwa mwezi.Safari za Rais hadi
muda huu kwa wastani niliotaja umegharimu sh.107100000000(Zaidi ya
Bilioni 107) ambazo ni karibia Nusu ya kodi ya laini itakayotozwa
Tanzania nzima kutoka kwa wamiliki milioni 22 wa laini za simu ambao
takwimu zinaonyesha milioni 8 kati yao hawana uwezo wa kutumia shilingi
1000 kwenye simu zao kwa siku.Wanatumia kwa Sms na kubip tu.Maskini
wanagharamia safari hizi ambazo mara nyingi Rais amekua akijitetea za
kutafuta wawekezaji zinaishia kuvuta hata wawekezaji ambao takwimu
zinaonyesha kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Interfaith Standing
Committee on Economic Justice and the Integrity of Creation mwaka jana
uligundua kuwa kwa wastani Tanzania hupoteza dollar billion moja
(takriban shs trilioni 1. kila mwaka kutokana na ukwepaji kodi, uhamishaji harama wa fedha na misamaha ya kodi.
Je ziara zote za Rais Kikwete zina manufaa na tija kwa taifa
letu?Katibu Mkuu wa CHADEMA na aliyekua mgombea Urais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania mwaka 2010 kwa tiketi ya CHADEMA Dr.Wilbroad Slaa
yupo nje ya nchi.Amesafiri mara chache na kwa kazi maalumu za kiofisi.
No comments:
Post a Comment