Ghana ilipiga hatua kubwa katika
kufikia kinyang'anyiro cha kombe la dunia baada ya kuicharaza Misri
mabao 6-1 katika mkondo wa mwisho wa mechi za kufunzu kwa kombe la dunia
mwaka 2014 nchini Brazil.
Asamoah Gyan aliingiza bao la kwanza ambalo lilifuatiwa na lengine la mchezaji wa Misri Wael Gomaa katika lango la Ghana.Bao lengine la penalti liliingizwa na Sulley Muntari na kuyafanya manne.
Christian Atsu naye alipata fursa na kuopnyesha nyota yake kwa kuingiza bao lengine huku akiiweka Ghana kifua mbele na kudhibiti mechi.
Mechi hiyo, ilikuwa imesemekana kuwa ngumu kwani timu hizo mbili zina wachezaji wazuri sana
Lakini kwa sasa ni kama wazi kuwa Black Stars wa Ghana wataabiri ndege ya kwenda Brazil baada ya ushindi wao mkubwa mjini Kumasi.
Hali ya wasiwasi ilijitokeza kabla ya mechi huku Ghana ikilalamikia FIFA kuwa inahofia kucheza mechi hiyo mjini Cairo kutokana na hali ya kisiasa ilivyo nchini Misri.
Huku ikiwa bado haijulikani mechi ya marudio itakochezwa, nia ya Ghana ilikuwa kupata alama nzuri zaidi ya Misri, nyumbani na hivyo ndivyo ilivyofanyika.
No comments:
Post a Comment