Zambia imetoa vibali vya
kukamatwa kwa wachezaji wake watatu waliokosa mechi ya kirafiki dhidi ya
Brazil mjini Beijing China. Hata hivyo Zambia ilishindwa na Brazil
mabao mawili kwa nunge.
Klabu ya DRC TP Mazembe ilisisitiza kuwa
wachezaji hao Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu na Nathan Sinkala
walijeruhiwa na kusababisha mgogoro kati ya shirikisho la soka la Zambia
na serikali ya Zambia.Hatua hiyo ilisababisha serikali ya Zambia kuingilia kati kwa kuwapokonya wachezaji hao pasi zao za usafiri ili kuwazuia kwenda kuchezea klabu yao mjini Lubumbashi.
Hata hivyo, wachezaji walifanikiwa kuvuka mpaka na wanaaminika kuwa nchini DR Congo.
Shirikisho la soka la Zambia limeandikia barua shirikisho la soka duniani Fifa, na kulalamika kuwa klabu ya Mazembe haikuwaruhusu wachezaji hao kushirki majukumu yao ya kimataifa.
Zambia ilishindwa kwenye mechi hiyo ya kimataifa mjini Beijing
Zambia ambao ni mabingwa wa kombe la taifa bingwa Afrika walikuwa wanashirki mechi yao ya kwanza wakiongozwa na kocha wao mpya Patrice Beaumelle, ambaye alichukua usukani siku nane zilizopita baada ya Herve Renard kucha kazi.
No comments:
Post a Comment