Tuesday, October 15, 2013

Ivory Coast yapiga hatua kwenda Brazil


Didier Drogba
Ushindi wa Ivory Coast dhidi ya Senegal umekuwa hatua muhimu ya kuelekea katika fainali za kombe la dunia.
Didier Drogba Mabao 3 yaliyofungwa na washambuliaji Didier Drogba, Gervinho na Salomon Kalou yametosha kuiongezea matumaini Ivory Coast ya kushiriki fanali za kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.
Goli la kufutia machozi upande wa Senegal lilifungwa kimiani na mshambuliaji wa NewCastle Papiss Demba Cisse.
Mechi ya mkondo wa pili itachezwa mwezi ujao nchini Morocco kwa sababu Senegal inatumikia adhabu ya kutochezea kwenye uwanja wa nyumbani.

Burkinafaso 3 Algeria 2

Penalti ya dakika za mwisho iliyopewa Burkinafaso katika mazingira ya kutatanisha iliiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Algeria.
Hadi dakika ya 85 matokeo yalikuwa magoli 2-2 kabla ya Burkinafaso kupata penalti iliyowawezesha kuondoka na ushindi mdogo.

No comments:

Post a Comment