Sunday, October 20, 2013

HIVI NDIVYO FACEBOOK INAVYOPATA PESA KUPITIA KWAKO


Kuwa na Akaunti ya Facebook ni kwa manufaa yako na manufaa ya Facebook

Facebook ambayo kwa sasa inapatikana katika lugha 70 ulimwenguni, ni mtandao wa jamii ambao unaongoza kwa kuwa na watumiaji wengi zaidi duniani. Wewe na mie kama watumiaji wa Facebook tunainufaisha kampuni hiyo ya Facebook, kwani kupitia kuitumia kwetu kunaiwezesha Facebook kuingiza mapato kwa njia ya moja kwa moja au nyingine.

Makala hii inakuchambulia namna ambavyo Facebook inaingiza "vijisenti" vyake:-


1. Kupitia Matangazo: Kwakuwa inao watumiaji wa mtandao wengi, ni rahisi kwa Facebook kushawishi watu binafsi na makampuni kutangaza bidhaa zao kupitia aina mbalimbali za matangazo yanayorushwa hewani na Facebook. Mfano , kampuni inaweza kudhamini POST yake, ili ionekane kwa watu wengi zaidi na mara nyingi. Pia kuna matangazo ya biashara ambapo unaweza kutengeneza tangazo lako la biashara na kulirusha hewani kupitia Ukurasa wako wa Facebook (Facebook Page).  Ili kutengeneza tangazo Facebook, unaweza kuenda sehemu maalum ukiwa Facebook imeandika 
CREATE AN AD.Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kulipia huduma hii.

Mfano wa Matangazo yanayoipatia fedha facebook
 
 

2. Salio maalum la Facebook ( Facebook Credit)

Ni kama vile unavyonunua salio la simu yako ili utumie salio hilo kupiga simu, ila kwa Facebook, unaponunua Facebook Credit, ni kwa ajili ya kuweza kutumia credit hiyo kulipia kucheza Games, au hata kununua vitu katika baadhi ya maduka yanayouza bidhaa zao ndani ya Facebook.

Unahitaji kuwa na Credit Card au Umejisajili na unayo akaunti ya Paypal ili kuweza kununua Facebook Credit.


3. Kupitia Kuuza bidhaa mbalimbali

Facebook inayo huduma ya kuuza bidhaa mbalimbali kwa mtindo wa "Gift" ambapo wewe mtumiaji unachagua nani unataka kumnunulia bidhaa , kisha unaenda kwa profile ya huyo unayetaka kumuuzia bidhaa. Utaona sehemu imeandikwa GIVE GIFT, ukibofya hapo utakutana na aina mbalimbali za zawadi na maelekezo. Hata hivyo huduma hii ya kutoa zawadi kwa watu haipataki kwa kila nchi. Inabidi ucheki Profile ya mtu husika unayetaka kumpa zawadi kuona kama GIVE GIFT ipo katika profile yake.
 

No comments:

Post a Comment