Yanga inaendelea kushikilia rekodi ya jumla baada ya ushindi mara 38, Simba 32, huku mara 32 zilitoka sare
Dar es Salaam. Huku zikiwa
zimesalia siku mbili, rekodi za miaka 13 iliyopita, zinaonyesha Simba
imeibuka na ushindi mara nyingi zaidi ya Yanga katika mapambano baina ya
timu hizo iliyopigwa siku ya Jumapili.
Simba na Yanga zitashuka Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam keshokutwa kukabiliana katika pambano la Ligi Kuu Bara mzunguko
wa kwanza.
Mwananchi lilifanya uchunguzi wake unaoonyesha
kuwa kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka huu Simba ina rekodi nzuri zaidi ya
kushinda siku ya Jumapili kuliko wapinzani wao, Yanga.
Rekodi hizo zinaonyesha kuwa katika kipindi hicho
Simba na Yanga zilikutana mara 20, ambapo kati ya hizo Simba iliibuka na
ushindi mara saba, wakati Yanga ilishinda mara mbili, huku mara 11
zikitoka sare.
Mechi zilizochezwa Jumapili baina ya Simba na
Yanga Juni 25, 2000 (Simba 2-1 Yanga), Agost i 18, 2002 (Simba 1-1
Yanga), Novemba 10 (Simba 1-0 Yanga), Novemba 12, 2000 (Simba 0-0
Yanga), Septemba 28, 2003 (Simba 0-0 Yanga), Novemba 2, 2003(Simba 4-1
Yanga).
Machi 31, 2002 (Yanga 3-0 Simba), Aprili 20, 2003 (Simba 1-1 Yanga), Aprili 17, 2005 (Simba 2-1 Yanga), Machi 26,
2006 (Simba 0-0 Yanga), Oktoba 29, 2006 (Simba 0-0 Yanga), Julai 8, 2007 (Simba1-1 Yanga), Aprili 27, 2008 (Simba 0-0 Yanga).
Oktoba 26, 2008 (Yanga 1-0 Simba), Aprili 19, 2009 (Simba 2-2 Yanga), Aprili 18, 2010 (Simba 4-3 Yanga).
(Julai 27, 2008) Yanga haikutokea uwanjani, Simba
ikapewa ushindi wa chee. Rekodi hizi zinajumuisha mechi za mashindano
mbalimbali ikiwemo Ligi Kuu Bara, Kombe la Mapinduzi, Tusker Cup,
lililokuwa Kombe la Chama cha Soka Tanzania (FAT) na Kombe la Kagame.
Hata hivyo, ukiondoa michezo baina ya timu hizo
iliyofanyika Jumapili, Yanga inaendelea kushikilia rekodi ya jumla baada
ya kuibuka na ushindi mara 38, Simba 32, huku mara 32 zilitoka sare.
Katika hatua nyingine, Kocha wa Yanga, Ernest
Brandts alisema, matokeo ya ushindi wa mabao 2-1 iliyopata kikosi chake
katika pambano la kirafiki dhidi ya Chipukizi ya Pemba yamekoleza morali
ya wachezaji wake kuhakikisha wanaibwaga Simba keshokutwa.
No comments:
Post a Comment