Baraza la Congress nchini
Marekani, limepitisha mswaada utakaowezesha serikali kuendelea ma
majukumu yake ya kifedha na kuongeza muda wake wa kulipa madeni
yanayoikabili.
Hatua hii imekuja masaa kadhaa kabla ya serikali kutumbukia kwenye mkwamo wa kifedha.Mswaada ulipitishwa kwa kura 285 dhidi ya 144 katika bunge la waakilishi ambapo wabunge wa Republican waliunga mkono mswaada huo shingo upande.
Afueni hii kwa serikali ya Rais Barack Obama imekuja masaa kadhaa kabla ya makataa ya kuongeza kiwango cha deni la serikali hadi dola trilioni 16.7.
Mswaada huo sasa utawezesha serikali kuendelea na majukumu yake ya kifedha na hata kuomba pesa zaidi kutoka katika hazina ya serikali hadi Februari tarehe saba.
Pia itawezesha serikali kupata pesa hadi Januari kumi na tano na kufungua mashirika ya kifedha katika majimbo na kuwaresha kazini maelfu ya wafanyakazi wa serikali.
Ikulu ya White house sasa imewataka wafanyakazi wa umma kurejea kazini leo.
Mswaada huo hata hivyo ni afueni ya muda na sio suluhu kwa matatizo ya bajeti ya serikali ambayo yaliwagawanya wanasiasa wa Republican na Democrats.
Baada ya mswaada kupitishwa, Rais Barack Obama aliwaambia waandishi wa habari kuwa atasaini mswaada huo na kuufanya sheria.
No comments:
Post a Comment