Tuesday, October 8, 2013

Huyu ndio mwimbaji STAR ambae dada yake Cristiano Ronaldo.

RONA 2
Haitokei kwa kila staa kuwa na ndugu wa damu ambae ni staa pia vilevile ila kwa mtu kama Cristiano Ronaldo ambae ni staa wa soka imetokea, dada yake (Kátia Aveiro) ni mwimbaji pia na sio tu wa kubahatisha ila kiukweli ni mkali.
Ni miezi miwili imepita toka Katia atoe single yake mpya Boom Sem Parar ambayo mpaka sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni moja laki nane ambapo video unaweza kuitazama hapa chini.

Katia alikua na ndoto za muziki toka siku nyingi ila muziki wenyewe alianza kuukomalia akiwa na umri wa miaka 27 na amekua akipata support ya Ronaldo toka mwanzo…. nakumbuka staa huyu wa soka wa Real Madrid alisema ‘nitakua mtu wa kwanza kununua album ya Katia atakapoanza muziki… ana sauti nzuri, utashangaa mwenyewe’
Kwenye sentensi aliyogusia kuhusu maisha yao ya nyuma, Katia amesema ‘hatukuzaliwa kwenye familia ya kitajiri lakini hatukuwahi kulala njaa wala kukosa viatu, sisi ni familia inayopendana sana… tunampenda Ronaldo ndio maana hata anapohamia kwenda kuishi kwengine ni lazima mmoja wetu aidha Mama au mimi aishi nae… tutafanya hivyo mpaka atakapokua na familia yake’
RONA1Hii picha ya pili wako na mama..

CHANZO-Milard ayo.com

No comments:

Post a Comment